GE2025 Polepole, Asante kwa ukweli wako kuhusu kiini macho cha Uchaguzi. Hoja ya tusishiriki, haina tija tena na Uchaguzi Upo!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi
Nimemsikiliza HP mwanzo mwisho, hoja zake ni za ukweli na za msingi sana kuhusu kiini macho cha uchauzi wa Tanzania.

Ushauri wake watu wasijitokeze kupiga kura mpaka kwanza upatikane muafaka wa kitaifa, ni ushauri tenge kama ulivyo uwanja tenge wa uchaguzi, it's a bit too little too late! kwasababu the game is already over!,watu waliisha maliza kazi kitambo, https://www.jamiiforums.com/threads...itaa-ccm-amekomba-almost-everything.2282068/, kilichobaki ni hiyo October 29 kwenda kuthibitisha kwa kukamilisha zile taratibu za kuhalalisha kwa kuitumia ile haki yetu ya kidemokrasia
kwa Thamani ya Kura Yako: Je Wajua Wewe Ndiye Mwajiri wa Rais wa JMT kwa Kura Yako na Kumlipa Mshahara Wake Yeye na Serikali Yake Yote kwa Kodi Yako?.

kwa hapa tulipo,hili lori semitrela lililobeba container la uchaguzi, liko mwendo kasi kwenye mteremko, huwezi kufunga breki likasimama ghafla, ukichuna breki za ghafla, the rate of change of velocity ni direct applied to the weight of the containers and takes place to the direction ya lori linakoelekea, hivyo ukichuna breki ghafla kwenye high speed kwenye huu mteremko mkali, kwanza tairi zitawaka moto kwa friction ya lami, gari litasimama ghafla, container zitapush mbele, lori itapinduka na kila kitu kitaparaganyika!.

Madam Watanzania tumekuwa tukifanyishwa igizo la uchaguzi na NEC huku tukifanyiwa kiini macho cha ushindi wa CCM kwenye uchaguzi siku zote na chaguzi zote bila kujua kuwa ni kiini macho, ila CCM ikishinda, hata kama ni kwa kiini macho!, si hua inatuletea maendeleo ya kuonekanika?, na Watanzania tunayaona kwa macho yetu wenyewe hayo maendeleo yanayoletwa na CCM?. Sasa tunachotaka taka ni nini?, uchaguzi mkuu huru na wa haki kwenye lindi la umasikini uliotopea, au igizo la uchaguzi wa kiini macho na kutupatia maendeleo ya kuonekanika?.

Wengi humu huwa wanakuwa conscious kuhusu uchaguzi mwaka tuu wa uchaguzi kama sasa, angalieni nilishauri nini kuhusu uchaguzi wa 2020 na nilishauri lini? Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Hapo angalieni nilisema nini kuhusu chaguzi zetu?.
Hivyo natoa wito kwa Watanzania, hiyo tarehe 29 October, twendeni tukaithibitishe tuu CCM, katika hilo igizo la mifumo, kama alivyosema Polepole!. Ile siku ile Nape alipoitoa siri hii, niliuliza kitu humu Pre GE2025 - Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?, sasa yanaporudiwa na Polepole, mnashangaa nini?!.

Haya mambo akina sisi, tumeyasema sana humu
 
Inasikitisha sana
 
Tupi
Tupige kura ili iweje sasa?...hebu tuondolee ujinga huo
 
Kaka Paskali
1. Kwanini unatetea uovu kwa kuhofia yatakayotokea???
2. Kwani wakati tunaingia kwenye vita ya KAGERA, hatukujua kuwa kuna watu watakufa?? Mbona tuliingia?? Tungeachia mipaka kisa kuna kufa???

Kwenye hili siafiki hoja yako
 
Mkuu Pasco kama unakiri kuwa alichosema HP ni kweli na sahihi kwa nini unawashauri Watanzania washiriki hii najisi?
 
Ushauri wako sikubaliani nao kwani uchaguzi ukifanyika hakutakuwa na maendeleo kama unavyoshauri; Utulivu katika nchi hautakuwepo,viongozi akiwemo Rais,hawatajiamini katika kutekeleza majukumu yao,wafadhili na wawekezaji hawatakuja na jumuiya ya kimataifa haitautambua uchaguzi huo.
Kwa hiyo miaka yote mitano hakutakuwa na mambo ya maana yatakayofanyika nk.
 
Kama ni kweriiiii tunaenda kwenye viunga vya uchaguzii kwa faida ya tlaatlaah na mwashambwa 😁 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…