Wanabodi
Nimemsikiliza HP mwanzo mwisho, hoja zake ni za ukweli na za msingi sana kuhusu kiini macho cha uchauzi wa Tanzania.
Ushauri wake watu wasijitokeze kupiga kura mpaka kwanza upatikane muafaka wa kitaifa, ni ushauri tenge kama ulivyo uwanja tenge wa uchaguzi, it's a bit too little too late!.
Lori la semitrela lililobeba container la uchaguzi, liko kasi kwenye mteremko, huwezi kufunga breki likasimama ghafla, ukichuna breki za ghafla, ghafla the rate of change of acceleration ni direct applied to the weight of the containers and takes place kuelekea the same direction, ukichuna breki ghafla kwenye mteremko mkali, tairi zitawaka moto kwa friction ya lami, gari inatupunga mwendo, container zitapush mbele, gari itapinduka na kila kitu kitaparaganyika!.
Madam Watanzania tumekuwa tukifa igizo la uchaguzi huku tukifanyiwa na CCM hiki kiini macho cha ushindi wa uchaguzi siku zote bila kujua kuwa ni kiini macho, na CCM ikishinda si hua inatuletea maendeleo ya kuonekanika, na Watanzania tunayaona kwa macho yetu wenyewe haya maendeleo yanayoletwa na CCM?.
Hivyo natoa wito kwa Watanzania, hiyo tarehe 29 October, twendeni tukaithibitishe tuu.CCM, maana uchaguzi tuliisha maliza kitambo,
Pre GE2025 - LGE2024 - Mwana JF, Be The First to Know CCM Ndie The Overall Winner wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 Kufuatia Ushindi Serikali za Mitaa。CCM Amekomba Almost Everything!
Tunafanyiwa na hiyo mifumo, kama ulivyosema!. Ile siku ile Nape alipoitoa siri hii, niliuliza kitu humu
Pre GE2025 - Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?, sasa yanaporudiwa na Polepole, mnashangaa nini?!.
Haya mambo akina sisi, tumeyasema sana humu