Polepole ataongea tena, tutapata uchungu zaidi lakini je, ni nani wa kutuokoa?

black abdu

Senior Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
157
Reaction score
214
Kichwa kimekuwa kizito baada ya kumsikiliza ndugu Polepole, kuna nyakati unakutana na habari ngumu usiyo na majibu hata unaona bora usingeijua...! Ni dhahiri kuwa haitatokea mgombea mkuu wa Nafasi ya Urais kwa sasa kujitoa, wala chama chake kutengua maamuzi, lakini pia hakuna mbadala sahihi wa kuweza kupokea kijiti endapo Watanzania wangeamua kufanya maamuzi magumu...!

Labda wananchi wangeandamana kudai mabadiliko, lkn nani anaweza kuwaunganisha wananchi kulitekeleza hilo?

Kwani haya yanayofanyika; ubadhirifu wa fedha na kujirundikia mali kwa wachache, nchi kupoteza fursa nyingi za kukua kiuchumi, mikataba ya ajabu, kuendelea kuzorota kwa huduma za kijamii.... hayawaathiri Jeshi letu? Je, hawawezi kuchukua nchi japo kwa muda?

Watanzania tumekuwa wanyonge, hatuna kauli wala maamuzi kwa nchi yetu, tunaowachagua watuongoze ni kama tu watawala, wanafanya wapendavyo na watakavyo.....!

Hadi lini? Polepole ataongea tena, tutapata uchungu zaidi lakini je, ni nani wa kutuokoa? Naishiwa Pawa..!
 
Rudini kwenye tatizo la msingi!
Tofautisheni vya Tanganyika/Zanzibar na vile vya Tanzania.
Tanzania ni cha wote! Sasa Ili uchungu uwepo WaTanganyika waambiwe jinsi halali yao inavyoliwa kiulaini!
Fanyeni hayo mkijua kuwa hao WaTanganyika hawajawai kupigania kilicho chao!
 
Back
Top Bottom