#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

Mihemko mibaya sana, tulikuwa hatujapata sample ya virusi ila saivi tunayo,
Tunaahidi tiba na chanjo tunazitafiti tupo maabara saivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiongelee ruzuku utaibua mengi...ila kubali tu wananchin hawana imani na nyie tena.
 
Usiongelee ruzuku utaibua mengi...ila kubali tu wananchin hawana imani na nyie tena.
Hapo ndipo nilipo na tatizo na wewe!Umetumia kipimo gani kufikia hilo hitimisho?Nami naweza nikasema wananchi hawana imani na JPM tena!
 
Sina ushabiki wa mambo ya kijinga lakini kwa hili mtoa mada umenigusa, then kwanini Khamis Mwinjuma aendelee kujiweka Quarantine wakati walitangaza kuwa wagonjwa watapelekwa Mloganzila? Inafikirisha sana!

ˡ ˡⁱᵏᵉ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Hapo ndipo nilipo na tatizo na wewe!Umetumia kipimo gani kufikia hilo hitimisho?Nami naweza nikasema wananchi hawana imani na JPM tena!
Mwenyekiti wa Chadema taifa (mb) alizomewa na wananchi wa hai. Na mahudhurio kiduchu kama karanga za kuonjeshwa.
 
Mwenyekiti wa Chadema taifa (mb) alizomewa na wananchi wa hai. Na mahudhurio kiduchu kama karanga za kuonjeshwa.
Unazungumzia wale walevi makada wa UVCCM waliotumwa na Sabaya?Huo upuuzi wenzako hawautumii tena maana umebuma!
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya BBC usiku huu hali ni Mbaya sana nchini Irani kusu ugonjwa wa Corona. Takwimu zinasema kila dakika kumi mtu mmoja anakufa na huko ktk wodi za wagonjwa Mahututi kumejaa wagonjwa na hakuna vifaa tiba.

Madaktari wamekata tamaa na hali iliyopo. Madaktari wengi wamekufa wakiwa wanapambana kuokoa maisha ya wagonjwa na wao kuambukizwa virusi vya korona.

Kitendo cha bwana Polepole kusema kuwa hawawezi kuzuia watalii kuingia nchini eti watakosa hela sio tuu ni kiburi cha madaraka pia ni kauli ya kujikinai kufuru kwa watanzania.

Kwa jinsi nilivyo ona taarifa ile hali ilivyo ktk mahospitali huko Irani ambako kiasi fulani wako mbele kimaendeleo huu ugonjwa sio wa kuufanyia mzaha kama hata mimi awali nilidhania ni ugonjwa wa kawaida tuu. Msdatkari walio hojiwa wanatia simanzi mno ktk utendaji wa kazi zao na wanaonekana hawana Promising future.

Kwa mahesabu rahisi tuu kama kila baada ya dakika kumi mtu mmoja anakufa, hivyo kila saa moja Irani wanakufa watu sita. Hii ina maana kuwa ndani ya masaa 24 watu 144 wanakufa huko Irani kwa takwimu za leo hii.

Watanzania wenzangu tuchukue tahadhari ya kutosha hali ikisha anza kuwa Mbaya hawa akina Polepole hatuta waona hadharani tena. Sisi maskini makapuku ndio tutakufa kama mbwa koko. Majuto ni mjukuu ndugu zangu hima tusifanye mzaha Dunia kwa sasa imo ktk tatizo baya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuleta shida kiuchumi sawa lakin kwann awausishe chadema na corona
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia mtu kazungumza pumba ndio kama hizi!!!! Unalinganisha kifo na pesa!!!! Labda sababu anajua yeye atakuwa mbali na hao watalii kwa hiyo poa tu!!! Hao watakao wahudumia hao watalii wakikamata ugonjwa na kufa potelea kwao!!!! Kwetu bei ya Maisha (Uhai) ni rahisi sana. Ingekuwa nchi ambazo raia wana nguvu juu ya seriklia yao huyu bwana alikuwa ajiuzuru haraka sana. Nchi kama Italia inategemea sana utalii lakini imefunga kila kitu au leo sisi ndio tunaijua pesa kuliko wazungu!!!!!??? Inasikitisha sana…...
 
Kj
Unazungumzia wale walevi makada wa UVCCM waliotumwa na Sabaya?Huo upuuzi wenzako hawautumii tena maana umebuma!
Hamkosi kisingizio,jamaa wanaweka wazi miaka ishirini treni ilikuwa haijakanyaga moshi JPM kawezesha barabara mbovu mbunge anakula bata mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…