Naomba nimfahamishi hili jambo Mr. Polepole. Jana alitoa hoja kuwa Tanzania hatuwezi kufunga mipaka sababu tutapoteza mapato tokana na utalii.
Hii sio sababu ya msingi Tanzania kutokufunga mipaka. Tanzania hatuwezi funga mipaka sababu inauchumi Tegemezi. Yaani tunategemea uchumi wa kimataifa.
Zaidi ya 70% ya bidhaa zinazotumika Tanzania zinatoka nje. Bandari yetu inaserve zaidi ya nchi 5. Tukifunga mipaka hata mwezi mmoja tu, uchumi unaweza poromika kwa hali ya hatari na serikali haitaweza pata fedha kuendesha hii nchi.
Hapa ndiyo tupate funzo kuwa nchi yetu bado ni Tegemezi. Hatuna jeuri ya kufunga mipaka hata siku moja.
Swala et tukifunga mipata tutapoteza watalii hii ni uongo au ufinyu wa fikra. Watalii kutoka nchi kama USA, Europe, Asia etc hawezi risk maisha yake kuja kwenye nchi ambayo anajua kuna korona na hata idadi ya waathrika ni vigumu kutambulika sababu ya uhaba wa vifaa vya upimaji nchi nzima.
Yaani mzungu kuja Tanzania sasa kwa utalii is like commiting suicide.
Kwa uzembe tulioonesha mpaka sasa hii secta ya utalii hapa Tanzania itayumba sana. Hata huu ugonjwa ukiisha watalii watakuwa bado na hofu ya kutembelea Africa hususan Tanzania.
Serikali ijipange kwa anguko kubwa la Uchumi. (2020-2021)
Sent using
Jamii Forums mobile app