#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

Akihojiwa clouds Humphrey polepole amesema wapinzani Ni sawa Corona.

Kauli hii ya kiongozi kijana inaweza tafsiriwa Kama kauli ya kiongozi aliyepoteza dira na ambaye kwake maisha ya watu wasio ccm si kitu bali binadamu sahihi ni mwanaccm.

Niwaomba viongoz wa chama tawala kuchukua hatua kwake na pia vyombo vya dola kumshughulikia kwani kumwacha aendelee na tabia hii kutasababisha wapinzani nao kutumia kauli Kama hizi kujibu mapigo na hivyo kusababisha mgawanyiko kwenye taifa.

Tukumbuke ishu ya MENDE kwa wenzetu...

**********
Amesema ukizuia Watalii kuingia Nchini kwa mwezi mmoja kutokana na #coronavirus italeta shida kiuchumi, hivyo ni kuomba Mungu ugonjwa huu uondoke. #COVID19 ni sawa na wapinzani Nchini

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, amesema "Tuna vituo Nchi nzima ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa ugonjwa wa virusi vya hivyo."

Kuhusu CCM kununua Wapinzani amesema "Si kweli kuwa CCM inatoa fedha kununua Wanachama wa upinzani bali inabidi wapinzani watazame jinsi wanavyoharibikiwa wenyewe ndani kwa ndani"

"Kuna mwanachama wa Mbowe anaitwa Paulina, aliondoka kwenye Chama kwasababu alikuwa anatakiwa kimahusiano na viongozi wake hivyo akaamua kuhama ili kuokoa ndoa yake lakini alivyohama wapinzani wakatafuta kisingizo kuwa amenunuliwa"

Ameongeza, "Chama cha Freeman Mbowe wanaiitana Bwana au Kamanda wao sio ndugu. Katika chama chetu huwa natumia sana neno ndugu na siyo Mheshimiwa kwa kwasababu sisi si kitu bila ya watu waliotupa dhamana"

Aidha, amesema "Hii tume ya Uchaguzi ni huru kabisa kama si huru mbona Halima Mdee na Joseph Mbilinyi walishinda? Mtu pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu tume ya Uchaguzi ni Umma na siyo Vyama Vya Siasa."

"Tume ya utumishi wa umma ndiyo inachakata majina 5 ya Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi na kumpelekea Rais ili ateue jina moja"

"Freeman Mbowe anataka tufanye maridhiano lakini sisi na wao hatufikirii pamoja kwenye kile wanachohitaji wananchi hadi sasa"

"Tangu nimekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM sijawahi kufanya mkutano wa hadhara.
Sisi kama CCM huwa hatufanyi mikutano ya hadhara kwenye majimbo yasiyoongozwa na wanachama wetu, mfano Mbeya ni Jimbo la Joseph Mbilinyi yeye huwa anafanya mikutano lakini akifanya anazungumzia jela kubaya"

"Godbless Lema hajawahi kutembelea miradi ya kimaendeleo Arusha Mjini na akifanya mikutano ya hadhara hazungumzii vitu hivyo bali yeye anazungumza kuhusu Jela tu. Kila tunachokifanya wanasema ni kibaya na sisi hatukatai kushauriwa kwasababu siyo maroboti lakini tangu tumeanza kupewa ushauri hatujawahi kupewa ushauri wa maana."
Hivi Polepole huwa anayaongea haya akiwa na akili timamu?Mbona statement kama za muhanga wa kilauri?
Unawezaje kusema watalii wakizuliwa nchi hii itakwama,Sisi siyo nchi ya viwanda tangu lini?Zamani tulikuwa nchi ya siasa ni kilimo,tukawa ya rukhsa,ikaja ukweli na uwazi,tukawa na ari mpya,nguvu mpya,kasi mpya na sasa hivi tulikuwa ya viwanda,Mara ghafla tumekuwa marafiki wa CoVid- 2019 ya mabeberu/watalii?Mnahamisha goli kila Mara na hamtaki kuulizwa.
Tume Huru kwa tafsiri ya Polepole ina vigezo gani na checks & balance yake ni chombo gani?Je, wapinzani ni Wananchi wa wapi?Wakisema wasiokuwa wanaCCM kuwa tunakosea mnawalinganisha na magonjwa,hiyo tafsiri yake siyo matusi/kashfa?
Kama mbunge alitakiwa kutoa rushwa ngono huko CHADEMA,aliwahi kwenda dawati LA jinsia ili sheria ichukue mkondo wake?Analinda wahalifu kwa kuhamia CCM?
Acheni kupotosha Wananchi.
 
Wakati wenzetu wanaanza kuugua corona wala hatukujishughulisha na kitu. Si tiba wala kinga...yaani tupo tupo tu.

Leo tumeanza pata corona..wala hatuwezi hata piga mikwara wageni wasiingie.mbaya zaidi hata hatuwazi kutafuta kinga wala tiba.tunakaa kusikiliza marekani na china wanafanya nini.

Tunapeana tu namna mpya za kusex....yaani swali linakuja sasa tuta sex vipi na corona. Yaani akili zetu ni za hovyo kiasi kwamba tunapozungumzia corona tunaihusisha na sex. Yaani tunaona kujikinga ni kutobusiana tu...tuna akili za kinyani mpaka leo.

Najuta kwanini sikusomea udaktari maana angalau ngetafuta wenzangu tuji organize tupambane na hii corona.siyo mijitu inawaza ngono tu all the time na kusubiri matamko from usa na china.
 
Afadhali ya Liquid kuliko chakubanga na Bashite
Sionagi tofauti kati yake na Pierre Liquid..
Nawachanganya hakika..

Everyday is Saturday..................... 😎

In God we Trust
 
Safari hata wangeruhusu ingekuwa ni kupoteza muda wa kufanya maendeleo.Hamna cha maana mgetueleza. Mfano kama vituo vya afya mia tatu na kitu vimejengwa ndani ya miaka minne mtatueleza nini? Hata kama hatuna chama.
Hakika ujinga ni mtaji mkubwa wa CCM, vituo kujengwa kisha hakuna waganga wala dawa kunatofauti gani na kuwa na maghala ya chakula na kuna njaa!
Acheni upumbavu wa kudanganyika na mambo ya propaganda kisha mnawapotosha hasa wale wenye elimu ndogo, nchi hii ni yao pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji21][emoji21][emoji21]
millardayo_B9q0bqzAr5p.jpeg
1584092525_1584092525-picsay.jpeg
 
Umenena mkuu ubarikiwe sana
Hakika ujinga ni mtaji mkubwa wa CCM, vituo kujengwa kisha hakuna waganga wala dawa kunatofauti gani na kuwa na maghala ya chakula na kuna njaa!
Acheni upumbavu wa kudanganyika na mambo ya propaganda kisha mnawapotosha hasa wale wenye elimu ndogo, nchi hii ni yao pia

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Wakati wenzetu wanaanza kuugua corona wala hatukujishughulisha na kitu. Si tiba wala kinga...yaani tupo tupo tu.

Leo tumeanza pata corona..wala hatuwezi hata piga mikwara wageni wasiingie.mbaya zaidi hata hatuwazi kutafuta kinga wala tiba.tunakaa kusikiliza marekani na china wanafanya nini.

Tunapeana tu namna mpya za kusex....yaani swali linakuja sasa tuta sex vipi na corona. Yaani akili zetu ni za hovyo kiasi kwamba tunapozungumzia corona tukihusisha sex. Yaani tunaona kujikinga ni kutobusiana tu...tuna akili za kinyani mpaka leo.

Najuta kwanini sikusome udaktari maana angalau ngetafuta wenzangu tuji organize tupambane na hii corona.siyo mijitu inawaza ngono tu all the time na kusubiri matamko from usa na china.
Kwanini unajumuisha Afrika nzima wakati kuna nchi za Afrika zilisitisha siku nyingi safari za nchi zilizoathiriwa?
 
Wewe wakati huo si ulikuwa kizingani ukapara samaki? Habari za siasa waachie wanao ijua siasa
Achana na habari za ukawa ambao walileta hii idadi. Mimi nataka urudi nyuma enzi zile Cdm ni Cdm kweli chinini ya Dk.

In God we Trust
 
Back
Top Bottom