Polepole hawezi kukemea utekaji na mambo mengine ya kihuni ya serikali ya sita. Maana yote yanayotendeka sasa yalitendeka pia 2015-2021

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aachie wadhifa huo wiki iliyopita, akikosowa vikali jinsi chama tawala cha mapinduzi, CCM, kilivyokiuka utaratibu kwa kumpitisha mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar, huku akitaja historia yake ya utumishi mpaka hatua aliyofikia.

Polepole amesema hakukubaliana kabisa na uamuzi wa CCM kuwapitisha wagombea urais hao mapema mwaka huu katika kikao ambacho hakikuwa na majukumu hayo huku akijisifia kwamba amekuwa karibu na serikali tangu mwaka 2000 na ameshiriki katika masuala mengi ambayo baadhi yalimfanya aende katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa.

"Na hapa nitawasema, wale wanaokuwaga wenyeviti wa kamati za maadili wanajua... Hili ni gumu kidogo.. unajua wakati mwingine unatakiwa ubomoe ili ujenge. Sasa, huu mchakato wa kupata wagombea kwa kweli tumeukosea, nimeongea na mzee mmoja, ndugu yangu, rafiki yangu nikamweleza, akasema pale bwana tulichemka.. Lakini sasa tunatokaje? Nikamwambia, kukiri tatizo ni sehemu ya suluhu.. nendeni mkarekebishe, mkipatie heshima chama chetu..." alisema Polepole.
 
Anaongelea kutekwa amesahau viroba vya mto ruvu bagamoyo?? Tukihoji kuhusu Saanane?Azori siyeye alikuwa mwenezi wa chama anaweza kutupa majibu??
Hoja na swali la msingi sana mkuu

Ila sibezi jitihada haifai kuendelea kuyanyamazia haya.
 
Kakata kuwa sehemu ya wahuni uku akiwa anamiliki KADI ya chama Cha wahuniii😁😁😁😁

Ameanza kwanza Kukataa wahuni na kuwaambia waache uhuni then anawasikilizia kama watendelea na UHUNI au watajirekebisha.
 
Kama Polepole aliongea pumba kwanini mfanye"Throating" ya Internet Kwa mitandao ya kijamii?mlikuwa mnaogopa nini?
 
Ha haaaa na wamehara kweli mpaka kufunga mitandao.......
 
Kuwa mchafu hakumnyimi haki ya kukemea uchafu. Swali la kijinga, kwanini Humphrey Polepole alipokuwa akitumika kama toilet 🪠 paper 🧻 🗞️ kwanini hamkumsema? Mlikuwa mkiunga mkono juhudi?
Polepole katukanwa sana humu, labda kama ndio umeanza kufuatilia siasa. Na huyo dada yake tulitaka atekwe na kupotezwa ili aje atoe mrejesho wa udhalimu alioukalia kimya wakati wa dhalimu magu.
 
muungwana ni mnafiki aliekubuhu 🐒
 
CCM is our enemy number one. Wapiganaji wake wakiasi sisi hatuwashambulii. Let them fight our archenemy!
 
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
 
Ni kosa kwa mlevi mstaafu kushauri madhara ya pombe?
Lini kaacha mambo ya ushenzi.
Wakati maiti zinaelea baharini tulipopaza sauti Polepole huyu huyu ndiye alikuwa anajibu kwa dharau.
Watanganyika mbona wasahaulifu namna hii?
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…