Polepole, kupanda ndege siyo anasa na wala kusafiri kwa barabara siyo kigezo cha kuwapenda masikini

Nikiwa Kijiwe Changu Cha kunywa Al Kasus Hapa Tandale Nimepelekwa mbali kifikra na mh.Polepole.....

NINAMFIKIRIA MH.MEMBE NA WALE WENZAKE kuhusu ule msaada wa VYANDARUA....

Mh.Membe akiwa waziri Mara tu baada ya kupanda NDEGE kutoka UGHAIBUNI na kurudi nyumbani tulifanikiwa kupata ule msaada wa VYANDARUA(ITN) kutoka kwa "mjomba" George Bush..........

Watu walipanda NDEGE na kugharamiwa kiasi kikubwa cha fedha za wavuja jasho wa nchi hii, eti lengo ni KUPEWA VYANDARUA, really?!!!!

Ndio mana nilipomsikiliza Polepole Akichambua UMUHIMU WA TANZANIA YA VIWANDA Kwan awamu hii huwa ninamuelewa anamaanisha nini........

Nina imani serikali hii itatufanikishia adhma yake ya kutujengea ama kushawishi UWEKEZAJI WA VIWANDA VYA DAWA ikiwemo VIDONGE DHIDI YÀ VIRUSI VYA UKIMWI(ARVs).
 
Tatizo hawezi kijieleza kwa kimalkia, hivyo anaona aibu ya kujidhalilisha. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
Hata China hajaenda nako kuna malkia? Tusishabikie ujinga
 
Hoja aliyoiraise Polepole ni kuwa mkuu wa nchi anapotumia gari kwenye ziara zake anakutana na wananchi wake na anapofahamu kero zao ndio anapata picha kamili ya nchi anayoitawala ipo vipi. Kuliko kuwa unaruka na ndege tu huku hujui kama wananchi wako wana kero zipi.
 

Facts.
 
Lugha anayoitumia Polepole Kuna hadhira anayoilenga.

Mbaya zaidi kwa hiyo lugha anaeleweka vizuri sana kwa kada husika.
 
Kuwapenda wananchi ni kutembea kwa miguu kama wao
 
Msafara una magari 80 helicopter
 
Anasafiri na barabara msafara wa magari zaidi ya 100 , Helcopter + Hospital(Ambulance) + Flying Doctors! Gharama zake ni zaidi ya 2B+ ambapo ni bora angepanda ndege gharama zingepungua maana wangeenda wachache tu!!
 
Kama angekuwa anajenga hoja mpaka kina Mnyika wanamshindwa, matumizi ya watu wasiojulikana na vyombo vya dola ni ya nini?
Wanaotukana na kuchochea maasi bila kujenga hoja. Wanao wakifanya ujinga hutandikagi au we bado mtoto?
Wapinzani wakileta utoto inabidi wafinywe kidogo japo yarisasi haifai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…