Polepole kuzungumza na Vyombo vya Habari Julai 17, 2025

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
230
Reaction score
793
Siku chache baada ya kutangaza kujiuzulu Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba na visiwa vya Jirani, Kada wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho wakati wa utawawala wa hayati Rais Magufuli, Humphrey Polepole ameitisha Press kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa Barua yake ya kujiuzulu hapo Julai 17.

Je, Serikali itaruhusu hiyo Press?
 
Kutoka Sweden?
 
Nilijua tu atafanya hivyo au kuhojiwa na media za kimataifa. Nilikuwa nasubiri siku na saa tu yatimie. Naona sasa yanakwenda kutimia.

ANGALIZO: Asitumie nafasi hiyo kupoza makali ya alichokisema kwenye barua yake.

Kwa maneno mengine, asimamie ukweli, wa alichokisema, ajibu shutuma na propaganda zinazoelekezea kwake na kamwe mkutano huo na waandishi usigeuka kuwa ni DAMEGA CONTROL kwa faida ya watesi wa Taifa hili.

Zaidi, afunguke na afafanue kwa kirefu na kwa mifano hai juu ya yote aliyoyasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…