Polepole kuzungumza na Vyombo vya Habari Julai 17, 2025

Wahuni walianza kupindisha habari; kaona anyooke nao.
 
Nimeogopa sana 🐼
 
Press aifanyie nje ya nchi kwani hapa anaweza kuzuiliwa na mamlaka. Labda kama atakanusha
 
CHawa mwashambwa aliahidi kuijibu barua yake, sasa ataijibu kabla ya press au anasubiri press kwanza.
 
Hivi amebahatika kupata mtoto huyu jamaa?
 

Saa za Afrika ya Mashariki, ina maana mkutano huu utafanyika nje ya mipaka ya taifa la Tanzania.

Amb. Humphrey Herson Polepole anataka kuongea kwa uhuru bila taarifa zake kufunikwa na wahariri wa vyombo pamoja na waandishi wa Tanzania ambao kwa namna fulani hawana uhuru wa kusambaza habari bila dola kuwaratibu nini kichapushwe, kipi kirushwe mtandaoni, network kukatika katika n.k

TOKA MAKTABA :

08 December 2024​

Prof. Kabudi sasa kuongoza Vyombo vya Habari vya serikali kushinda propaganda / information war kuelekea 2025 na mbele zaidi​

Uteuzi wa Profesa Palamagamba Kabudi, ni hatua nzito ya serikali kujipanga kushinda vita ya habari yaani propaganda.

Vyombo kama TBC, TBC radio, Habari Leo Daily News, Idara ya Maelezo vimekuwa vikisinzia kuitetea serikali ya awamu ya 6 kiasi ya kuwa vyombo vya mitandao ya kijamii vimeibuka washindi katika kuunda sura (ku shape ) ya yanayoendelea nchi huku vyombo vya umma vikikosa wasikilizaji, wasomaji na wachangiaji (comments) iwe katika lugha ya KiSwahili au Kiingereza

Hivyo hatua ya uteuzi wa leo ni kujaribu kurudisha mizania kuegemea upande wa serikali na chama tawala au angalau kuweka mzania sawa balanced kutoka hali ya sasa ambapo vyombo vya habari vya umma vya kieletroniki, radio, televisheni vimeshindwa vita hii ya habari information war

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Profesa Palamagamba Kabudi sasa kuendeleza propaganda :
Vita ya habari au information war ni zana muhimu kutetea uhalali wa maamuzi, matukio na mafanikio


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…