GE2025 Polepole: Tunaendaje kwenye Uchaguzi wakati Mpinzani wa Kweli yuko Gerezani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Aliposhangilia zile risasi hakuwa mpinzani wa kweli?
 
Yupo sahihi
mpinzani og yupo jela
simba wa Africa!
Pole pole aache unafiki. Hivi kweli anaamini kuwa Lisu ni mpinzani wa kweli ilihali anajua kua alipata 13%ya kura uchaguzi uliopita?
Labda atoke hadharani na aseme kuwa ile 13% aliopata Lisu na kiti kimoja cha Ubunge waliopata CHADEMA hayakuwa matokeo sahihi. Yeye ni dhahiri huenda akawa anajua mengi zaidi tatizo lake anachagua yakusema. Sema yote tujue exactly kilichotokea uchaguzi 2020 wewe ukiwa mwenezi unaetembelea vietee
 
Akifanya yale ya Ibrahim mbona ndiyo shimo kabisa la CDM, kwani cuf ipo?.
 
Hivi kufanya siasa kwa akili ni kukubali kuwa lapdog ?!

Basi siasa haina faida
Kumjua mpinzani wako strength yake na weakness yake na kuja na njia mbadala ya kuonyesha jinsi gani utakavyoleta mabadiliko. Kwa sasa unaona CHADEMA wanaweza kushinikiza NRNE au kupambana na kesi ya kiongozi wao?
 
Samia anataka kuforce King, hapo kuna faida na madhara ila madhara ni mengi zaidi.

Yaani Katiba ilimpa nafasi yeye kubeba mzigo ili kumalizia safari baada ya mgombea mweza wake wa Urais kutwaliwa, ila sasa mzigo huo kaufanya wa kwake amegoma kuutua na kuukabidhi kwa wenyewe.

Swali kwa watanganyika je hii ni sawa? Swali kwa wana CCM je hii ni sahihi?
 
Kumjua mpinzani wako strength yake na weakness yake na kuja na njia mbadala ya kuonyesha jinsi gani utakavyoleta mabadiliko. Kwa sasa unaona CHADEMA wanaweza kushinikiza NRNE au kupambana na kesi ya kiongozi wao?
Kutumia uparattus za umma kumdhibiti mpinzani wako kupitia weakness za katiba siyo ujanja bali ubinafsi. Hasa maslahi ya kundi dogo na siyo future ya nchi. Bahati nzuri ni Tanganyika kila kitu ni yes.

Ccm wanatamba kama moja ya chama kikubwa Africa. Lakini hawako tayari kwa free & fair election !!. Ukubwa gani sasa labda wa uoga. Acha mama ashindane na kina Tadea, updp & Co. Huko ndiyo waonyeshe Ukubwa.
 
Jamaa ana hoja.
 
Sasa kususia uchaguzi ndiyo kutafanya marekebisho ya katiba? Au kitazuia chama tawala kisitumie vyombo vya dola au mahakama kwa manufaa yake?
 
Unamwita Mpizani wa kweki!! wakati 2020 election amepata 13% ya vote, na chadema wapata seat moja kwenye bunge.
Polepole kwa atuambie walimfanyaje mpizani wa kweli 2020
Kwanini muendelee kuwabyanganya ushindi wao huku mnajua hawawezi kufikisha hata 13% ?!

Weka tume huru uone kati ya Cdm and Ccm nani anavuka 50% !!.

ANC ni chama kikubwa kuliko Ccm kwa kila kitu. Hakipori kura za wapinzani wao.
 
Mbowe alikua mwana diplomasia mbona alipewa kesi ya ugaidi?
 
Mngese huyo,hana tena mazito ya kutikisa nchi,kaungana na makahaba wa dayaspora akina maria sarungi na mange kimambi
Upinzani wa kweli unapimwaje?
 


Umoja ni nguvu, tutahinda!
 
Kwani wakati yeye NI karibu mwenezi mwaka 2020 CCM iliingiaje kwenye uchaguzi wakati wagombea weeengi upinzani walipoenguliwa sababu ya kukosea kujaza fomu,si alibariki huyu kupita bila kupingwa
 
Wewe mwenzetu uko dunia nyingine kabisa!!
 
mazingira ambayo nchi haiko moja tumegawika wengine hawafanyi Siasa kwasababu wamefungwa mikono, unapataje amani unakwenda kwenye uchaguzi mpinzani wa kweli yupo jela? Haiwezekani."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…