GE2025 Polepole: Tunaendaje kwenye Uchaguzi wakati Mpinzani wa Kweli yuko Gerezani?

GE2025 Polepole: Tunaendaje kwenye Uchaguzi wakati Mpinzani wa Kweli yuko Gerezani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwahiyo kushiriki ndio kutasaidia nini sasa?
Kutasaidia kujua chama kina ushawishi kiasi gani katika kuchukua hatamu ya nchi.
Hata wakati TANU ilipoingia kwenye uchaguzi wa kura tatu, kuna viongozi ndani ya chama waligoma na kukawa na upinzani ndani ya chama lakini Mwalimu Nyerere alisimama imara na kukiingiza chama kwenye uchaguzi na hatimae walifanikiwa.
 
Humphrey Polepole akizungumza kwa njia ya Mtandao usiku wa Agosti 13 amesema; "Mama Samia Mungu atamgusa, nchi hii ni kubwa zaidi kuliko yeye na kwamba dhamana ilimtaka yeye ndiyo awe Rais wa nchi yetu baada ya aliyekuwa Rais kutwaliwa na Mungu. Kwahiyo ana Haki ya kulinda maslai mapana ya nchi ya Tanzania, asijitazame yeye kwanza."

"Tunakwenda kwenye Uchaguzi katika mazingira ambayo nchi haiko moja tumegawika wengine hawafanyi Siasa kwasababu wamefungwa mikono, unapataje amani unakwenda kwenye uchaguzi mpinzani wa kweli yupo jela? Haiwezekani."

Akamtoe Ili agombee nae
 
Mbowe ni mwanadiplomasia mzuri ila aliposhupalia shingo na kuleta ubabe ndiyo akapewa kesi.
Ubabe gani alileta wakati alikua anakomaa na maridhiano huku wenzake wakimpinga!

My point is CCM hawana huruma uwe mpole au mkali watakunyoa nywele.
 
Kutasaidia kujua chama kina ushawishi kiasi gani katika kuchukua hatamu ya nchi
Utajuaje wakati kabla hata ya kura kupigwa 50% ya wagombea udiwani na ubunge wanakua wameshakatwa kama 2020!!

Chadema inakubalika sana na hata Samia anajua hilo unaweza ona reception kwenye mikutano yao hakuna wasanii ila viwanja vinatapika.

Uwanja ukiwa fair hata CCM ikishinda ujue itakua 45% pekee!! Na almost nusu ya wabunge wangeenda nyumbani.
 
Kesi ya Lisu inafanafa sana na ile ya Yesu Kristo.
Waliomshtaki Kristo walishindwa kujua ni makosa gani wanamshtaki nayo!
Wanaomshtaki Lissu hawajia wamemshtaki kwa kosa gani!
Kristo alikufa msalabani kwa makosa ambayo hayakuwepo.
Lissu wanataka kumhukumu kwa kosa ambalo halipo!
Yesu Kristo alishinda mauti kwa kuwa Mungu wa Milele alikuwa nae.
Lissu atashinda yote kwa kuwa Mungu yupo nae siku zote
 
Shetani hakuwahi kuwashinda watu wa Mungu hata mara moja, Lissu pamoja na mateso yote atashinda maumivu haya . Amina
 
Utajuaje wakati kabla hata ya kura kupigwa 50% ya wagombea udiwani na ubunge wanakua wameshakatwa kama 2020!!

Chadema inakubalika sana na hata Samia anajua hilo unaweza ona reception kwenye mikutano yao hakuna wasanii ila viwanja vinatapika.

Uwanja ukiwa fair hata CCM ikishinda ujue itakua 45% pekee!! Na almost nusu ya wabunge wangeenda nyumbani.
Nina uhakika haitakuwa hivyo, tatizo muheshimiwa Lisu kataka ku-force King na kujaribu kuona huyu mama atafanya nini?

Chama dola kiwe fair ili iweje? Madaraka yana ladha yake ni vigumu kuyaachia hivihivi.
 
Mbona JK alikua fair, alibana kwenye urais ila ubunge, udiwani akaachia kila mtu ajipambanie?
Yetu macho, usishangae hata Mpina akakatwa kugombea Urais!!
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa si sawa na uchaguzi wa 2020.
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ni sawa na zama za JK tu.
 
Back
Top Bottom