Polepole: Ukiwa mwadilifu tegemea vikwazo kutoka kwa wahuni

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Pasi na kupepesa macho dhidi ya wahuni sikia mambo:

Your browser is not able to display this video.


"Kama si fitna, zengwe au kurogwa tegemea kujikuta ana kwa ana na wasiojulikana."

Ama kwa hakika wahuni si watu wazuri!

Tumesikia wakitishiwa watu kuuwawa. Uthibitisho kuwa wahuni huupiga mwingi hadi nje ya CCM.

Tunaporumbana nao kuhusu bandari zetu, maneno ya Polepole aka kiroboto, yanaishi:

"Usiku ni kuwa macho sana!"
 
Yeye mwenyewe muhuni tu kama hao wenzake.

Tofauti yetu na nchi zingine ni kujikita kuwajadili watu badala ya hoja zao.

Hapa ndipo tunapofeli hali wenzetu kama Kenya wakipeta.

Urafiki wa kudumu katika siasa ni katika hoja si katika personalities.

Hatujiulizi kulikoni Raila, Karua, Uhuru, Kalonzo nk leo pamoja au kulikoni hao wote na Ruto waliwahi kuwa washirika katika mapambano?

Tungali na safari ndefu sana!
 
Hichi kizee kilipaswa kusema hayo maneno wakati wa Magufuli, badala yake kikawa kinaruka sarakasi na kukatika muziki Ikulu kwa shangwe. Kwa sasa nacho kimeshikwa pabaya na kubwabwaja tu.
Pole pole ni irrelevant kwa siasa za awamu hii,atulie ale matunda ya ubalozi wake
 
Kumbe mnamwita kiroboto mie nilijua CHAKUBANGA
 
Kwenye bandari msimamo wake upoje!?
 
Huyo mwamba ni threat ndio maana wanamsogeza mbali
Leo wanatishwa vinara wa kupinga mkataba wa DP World, wabongo hawana Cha kuokota toka hata kwa Polepole bali kumnyanyapaa. Ndiyo maana CCM yakisema yatatutawala kwa miaka 100.
 
Kwenye bandari msimamo wake upoje!?

Kwamba waadilifu hutishwa, huundiwa mazengwe, fitina huwahusu bIla kuwasahau wasiojulikana? Kumbe kama waadilifu yanawasibu hayo, msimamo wake kuhusu bandari mbona utakuwa uko wazi ndugu?
 
Shida ni katika mazingirw wanayo tugeuka yaan mtu akinyimwa tonge anakua upande wa wananchi akipewa anasapoti mateso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…