GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Usiku wa saa Sita, Humphrey Polepole amedai kuwa; "Watu wameruka ukuta wa nyumbani kwa dada yangu Bahari Beach. Wamemwambia dada yangu wamefuata taarifa."

"Ninakwenda kujiridhisha. Sina tatizo kabisa, nilishamwambia Mungu wa mbinguni na anajua nina yeye tu."

Andiko lake limekuja masaa kadhaa kuelekea mkutano wake na Vyombo vya Habari baada ya kutangaza kusogeza mbele kutoka Julai 17 hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025 saa 5:00 asubuhi.

IMG_5567.jpeg

Mkutano huo unatarajiwa kutoa ufafanuzi kuhusu barua yake ya kujiuzulu Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba.

==
Updates

"Kwenye saa tano usiku dada yetu, dada yangu mkubwa alimpigia simu mama yangu akamwambia kuna watu wameruka ukuta wameingia nyumbani kwake anaishi huko Bahari Beach. Na wakasogea mpaka kwenye nyumba wakamuambia wamefuata taarifa," ameeleza Polepole kwenye video aliyoiachia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Toka wakati huo saa tano, dada yangu simu yake haipokelewi. Tumejaribu kwenda pale nyumbani, watu wameona kuna magari, kuna Landcruiser, kuna Noah ambazo zilikua maeneo ya nyumbani mpaka muda huo wa saa tano na baadae," aliongeza zaidi.

"Na watu wengine ambao sio jamaa zangu [walionekana]. Kwa sababu dada yangu anakaa peke yake, wanafungua geti la nyumbani wanaingia wanatoka, baada ya muda tena wanarudi. Mimi nilitaka kusema, mimi sikai kwa dada yangu, na kama kuna mtu ananitafuta mimi, namba zangu zinapatikana," alifafanua zaidi Polepole ambaye amesema ataongea na Umma leo saa tano.

Soma zaidi
 
Polepole aache uzushi.


Hivi una kitu chochote cha kukufanya utoe kauli kama hiyo, au ni ule uropokaji wa mapunguani wa akili.

Kama ungekuwa na akili japo kidogo, ungeweka taarifa ya kweli uliyo nayo wewe ili kuthibitisha yaliyosemwa na Poepole ni uzushi.

Kama ni wewe uliyeruka ukuta, na sababu ya kuruka huo ukuta siyo hiyo aliyoisema Polepole, utuambie.
 
Kwani Polepole yupo dar hapa?
Yupo na hana stress ya kufanywa chochote
Ulijua yupo wapi?
huyu si alikuwa Sweden, kafika Dar lini?

Kwa usalama wake Polepole anapaswa aende akaishi nje ya Nchi hii kwa sasa hadi hapo baadaye hali itakapotengemaa.
Wenzake Wana hasira naye Sana, ametoboa jahazi lao wanalosafiria na Sasa chombo chao kinakwenda mrama, matumaini ya kufika pwani wakiwa salama yamepotea.

Ajifunze Sana Jambo hili kwa Sasa: Unconventional Methods of Inflicting Harm Upon Another Person.

Hii itamsaidia kuongeza siku zake za kuishi.
 
Wakuu!

Usiku huu Humphrey Polepole amedai kuwa; "Watu wameruka ukuta wa nyumbani kwa dada yangu Bahari Beach. Wamemwambia dada yangu wamefuata taarifa."

"Ninakwenda kujiridhisha. Sina tatizo kabisa, nilishamwambia Mungu wa mbinguni na anajua nina yeye tu."

Andiko lake limekuja masaa kadhaa kuelekea mkutano wake na Vyombo vya Habari baada ya kutangaza kusogeza mbele kutoka Julai 17 hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025 saa 5:00 asubuhi.

View attachment 3409323

Mkutano huo unatarajiwa kutoa ufafanuzi kuhusu barua yake ya kujiuzulu Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba.
Kazi ipo! Polepole mwaga mboga tunakusubiri
 
Back
Top Bottom