GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Alishaondoka Cuba muda mrefu tu kabla hata ya kuresign
Anapaswa aondoke hapa nchini kama yupo hapa, ni hatari kubwa sana kwa usalama wake. Utawala wa dhalimu wa nchini Urusi Watu kama yeye huwa wanakuwa eliminated by poisoning, achukue tahadhari kubwa sana, Utawala uliopo hapa kwetu una uswahiba mkubwa Sana na Utawala wa Urusi. Akumbuke kwamba ndege wafananao huruka pamoja!
 
Wakuu!

Usiku huu Humphrey Polepole amedai kuwa; "Watu wameruka ukuta wa nyumbani kwa dada yangu Bahari Beach. Wamemwambia dada yangu wamefuata taarifa."

"Ninakwenda kujiridhisha. Sina tatizo kabisa, nilishamwambia Mungu wa mbinguni na anajua nina yeye tu."

Andiko lake limekuja masaa kadhaa kuelekea mkutano wake na Vyombo vya Habari baada ya kutangaza kusogeza mbele kutoka Julai 17 hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025 saa 5:00 asubuhi.


Mkutano huo unatarajiwa kutoa ufafanuzi kuhusu barua yake ya kujiuzulu Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba.

Soma zaidi
Wenzetu Dada zao wanaishi Ushuani.
 
Mkuu timu uuwaji kuteka na kutesa huyo. Ndiyo michango yao humu
Hivi una kitu chochote cha kukufanya utoe kauli kama hiyo, au ni ule uropokaji wa mapunguani wa akili.

Kama ungekuwa na akili japo kidogo, ungeweka taarifa ya kweli uliyo nayo wewe ili kuthibitisha yaliyosemwa na Poepole ni uzushi.

Kama ni wewe uliyeruka ukuta, na sababu ya kuruka huo ukuta siyo hiyo aliyoisema Polepole, utuambie.
 
Back
Top Bottom