GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
MBona mnaongezeka sana,gwajima boy njoo huku umepata mwenzako
 
🔴 Watu wavamia nyumbani kwa dada wa polepole, wafuata taarifa

Balozi Humphrey Polepole ametoa ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Amesema watu wameruka ukuta nyumbani kwa dada yake huko Bahari Beach. Walipokutana naye, wakamwambia wamekuja kufuata taarifa kuhusu Polepole mwenyewe.

Kupitia kauli yake mwenyewe, ameandika:

"Watu wameruka ukuta wa nyumbani kwa dada yangu bahari beach. wamemwambia dada yangu kuwa wamefuata taarifa.
ninaenda kujiridhisha.
sina tatizo kabisa, nilishamwambia mungu wa mbinguni na anajua kuwa nina yeye tu." Ameandika

Tukio hili limeibua maswali mengi.
Je, kuna mtu au kikundi kinamfuatilia Polepole?
Ni kwa sababu gani hadi ndugu wa karibu wanaanza kulengwa?

👀 Watu wameanza kuhoji:
➡️ Huu ni ujumbe wa vitisho au ni hila ya kisiasa?
➡️ Je, huu ni mwanzo wa mambo makubwa yanayokuja?

🗣️ Tuambie maoni yako — unadhani nini kinaendelea hapa?
👇👇👇

#polepole #usalama #habarimpya #halisimax #baharibeach #taarifa #tanzania #siasa #familia #halisinewsflash #tanzania #halisimediatz
 

Huyo dada yake hana Rotweliier, Pitbull, German Shepherd, au hata Koko?
 
Anyways...
Ebu ngoja tuone mwisho wa haya yanayo zidi kujiri
 
HUmu akili zenu mlipewa zile za mwisho hafifu unadhani unatoa tu taarifa .
Lazima uwe na akili . Watu wanafuatiliwa majumbani mwao wanatishiwa kuuwawa, kuuliwa kwa ndugu zao anamengi yakusema ila kisa kuogopa kutekekwa kwa familia yake anakaa kimya anaonekana mzushi,gwajima ni inshu ingine anaulinzi lukuki sio polepole ,. Akisema kasema
 
Mkuu wakati mwingine angalia mleta hoja katumia jina gani! Wengine ni wakuwapuuza tu.
Waungwana wanasema "never argue with a fool people might not notice the difference ".
Utakuwa umenipata!
 
Siasa za chukuwachakomapema;-

Vitisho kwa kutumia nguvu za Dola na wahuni, ufisadi, kutokuwa na hoja, kutokuwajibika, ulevi wa madaraka, wizi, uroho, ubinafsi, UJINGA, uchawa, undorobo....
Wanatapatapa, mwisho wao?!
 
Kumeanza kukucha sasa.Leo ni zamu ya pole pole sasa...
 
Huyo jamaa ni mjinga mno anafikiri hao waliopotea au kushambuliwa akina Dr Kitima hawamjui Mungu.

Kama kaamua kujilipua aache kutiatia huruma,apambane na uhalisia ni hafiki popote pekee yake.

Angejikalia zake huko huko akifanya ukosoaji wake,sasa hivi hawezi kutoka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…