GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wahuni wapelekewe moto 😅😅😅
 
Kwani amesharudi kutoka Havana?
Kama amesharudi na yuko salama basi,nahisi tu hakuna jipya!
Yalishapangwa kutuhadaa raia.
 
Kuna jambo linakuja ....
 
Mungu akufanyie wepesi saa tano ikukute ukiwa salama salimini na usifanyiwe ya Nape na wahuni unaowasuta🙏🏼🙏🏼🙏🏼
 
Polepole atoa taarifa kuwa watu wamevamia nyumbani kwa dada yake, aeleza simu za dada yake hazipatikani.

"Kwenye saa tano usiku dada yetu, dada yangu mkubwa alimpigia simu mama yangu akamwambia kuna watu wameruka ukuta wameingia nyumbani kwake anaishi huko Bahari Beach. Na wakasogea mpaka kwenye nyumba wakamuambia wamefuata taarifa," ameeleza Polepole kwenye video aliyoiachia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Toka wakati huo saa tano, dada yangu simu yake haipokelewi. Tumejaribu kwenda pale nyumbani, watu wameona kuna magari, kuna Landcruiser, kuna Noah ambazo zilikua maeneo ya nyumbani mpaka muda huo wa saa tano na baadae," aliongeza zaidi.

"Na watu wengine ambao sio jamaa zangu [walionekana]. Kwa sababu dada yangu anakaa peke yake, wanafungua geti la nyumbani wanaingia wanatoka, baada ya muda tena wanarudi. Mimi nilitaka kusema, mimi sikai kwa dada yangu, na kama kuna mtu ananitafuta mimi, namba zangu zinapatikana," alifafanua zaidi Polepole ambaye amesema ataongea na Umma leo saa tano.
 
Nashindwa kuelewa ukiacha kazi unachukiwa na pia ukiendelea kufanya kazi pia unachukiwa nashindwa kuelewa hawa watu wanataka nini?
 
Hivi kwa nini wasipuuzie hao wanaoitwa wasio julikana!
 

Binafsi siwezi kumwamini huyu jamaa hata siku moja, labda kama mbele ya safari atabadilika !
 
Nchi hii yetu sote. Ebu achane Urwanda huo. Polepole anasema kweli. Saa 5 atalipua hao wanaofanya vitendo vya kihuni.
 
Yaani km unacho cha moto unawamiminia za kutosha washike adabu. Unaruka ukuta si ujambazi huo
 
Si ndio yeye wakat wa magu muanzilishi alikuwa happy na kujibu ovyo leo vip? Akitekwa mama yako ndio utajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…