GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

GE2025 Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hivi una kitu chochote cha kukufanya utoe kauli kama hiyo, au ni ule uropokaji wa mapunguani wa akili.

Kama ungekuwa na akili japo kidogo, ungeweka taarifa ya kweli uliyo nayo wewe ili kuthibitisha yaliyosemwa na Poepole ni uzushi.

Kama ni wewe uliyeruka ukuta, na sababu ya kuruka huo ukuta siyo hiyo aliyoisema Polepole, utuambie.
Usijichoshe mkuu kumaliza muda wako watu wa hivyo ndio mtaji wa chama tawala
 
Naona sasa Polepole anaanza kunyweshwa muarobaini alioshiriki kuukoroga enzi hizo akiwa na mshikaji wake Magufuli.

What goes around comes right back around... wahenga walisema.

Kama kweli Polepole uko nchini si uende Polisi ukaropoti tukio?
 
Naona sasa Polepole anaanza kunyweshwa muarobaini alioshiriki kuukoroga enzi hizo akiwa na mshikaji wake Magufuli.

What goes around comes right back around... wahenga walisema.

Kama kweli Polepole uko nchini si uende Polisi ukaropoti tukio?
View attachment 3409562

Kwani kaitwa Police? Kwani police wamesema ndo wameenda kwa Dada yake? Au una kiherehere tu?
 
Naona sasa Polepole anaanza kunyweshwa muarobaini alioshiriki kuukoroga enzi hizo akiwa na mshikaji wake Magufuli.

What goes around comes right back around... wahenga walisema.

Kama kweli Polepole uko nchini si uende Polisi ukaropoti tukio?
View attachment 3409562
Dada ake ameolewa au alikua anaishi peke yake?
 
Kila jambo na wakati wake.
Hakuna aliyezaliwa mwema kabisa bila doa au m-baya kabisa bila jema lolote.

Ili siku ikamilike kuna masaa ya mwanga na ya giza pia.
Hivyo relax....mfuatilie Polepole saa tano.
Hana jipya yeye nae ni muasisi wa hayo labda aje aseme sanane yupo wapi?
 
Aiseee, huu uhuni hawataki kuuacha mpaka muda huu, kweli tulipata kuambiwa hakuna aliye salama. Mwl Nyerere alipata pia kutuambia dhambi ya ubaguzi ukiisha kuitenda kamwe haitakuacha salama, walianza kubaguliwa Watanzania walioitwa wapinzani, sasa ngoma inahamia ndani kwa ndani, na Mwl akasema naomba Mungu anisamehe, lakini mkiisha itenda dhambi ya kubaguana, naomba iwatafune kweli kweli, sasa naona imeanza
 
Anapaswa aondoke hapa nchini kama yupo hapa, ni hatari kubwa sana kwa usalama wake. Utawala wa dhalimu wa nchini Urusi Watu kama yeye huwa wanakuwa eliminated by poisoning, achukue tahadhari kubwa sana, Utawala uliopo hapa kwetu una uswahiba mkubwa Sana na Utawala wa Urusi. Akumbuke kwamba ndege wafananao huruka pamoja!
Unaifahamu Kuba wewe in Polepole's voice🤣🤣🤣
 
🔴 Watu wavamia nyumbani kwa dada wa polepole, wafuata taarifa

Balozi Humphrey Polepole ametoa ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Amesema watu wameruka ukuta nyumbani kwa dada yake huko Bahari Beach. Walipokutana naye, wakamwambia wamekuja kufuata taarifa kuhusu Polepole mwenyewe.

Kupitia kauli yake mwenyewe, ameandika:

"Watu wameruka ukuta wa nyumbani kwa dada yangu bahari beach. wamemwambia dada yangu kuwa wamefuata taarifa.
ninaenda kujiridhisha.
sina tatizo kabisa, nilishamwambia mungu wa mbinguni na anajua kuwa nina yeye tu." Ameandika

Tukio hili limeibua maswali mengi.
Je, kuna mtu au kikundi kinamfuatilia Polepole?
Ni kwa sababu gani hadi ndugu wa karibu wanaanza kulengwa?

👀 Watu wameanza kuhoji:
➡️ Huu ni ujumbe wa vitisho au ni hila ya kisiasa?
➡️ Je, huu ni mwanzo wa mambo makubwa yanayokuja?

🗣️ Tuambie maoni yako — unadhani nini kinaendelea hapa?
👇👇👇

#polepole #usalama #habarimpya #halisimax #baharibeach #taarifa #tanzania #siasa #familia #halisinewsflash #tanzania #halisimediatzView attachment 3409470
Uki deal sana na wakosoaji, unaongeza wakosoaji. Kila wanavyoumia/kufa/kufungwa/kupotea,, unaongeza makovu ya hasira, chuki, visasi vya ndugu, watoto, wajane, wapambe na marafiki wa wahanga.

Hii ni kanuni sawa na historia ya ukuaji wa ukristo. Mtawala wa Rumi mfalme Nero aliuwa sana WAKRISTO, na wakosoaji wake ,, lakini kadiri ya mauaji ndivyo ukuaji wa ukristo ulivyoongezeka.

Taifa hili ni rahisi sana kulitawala bila mauaji mabaya hivi. Kumbukumbu zangu, Nyerere alijiepusha sana na umwagaji damu pamoja na kukosolewa. Tena yeye sio kukoselewa tu, ila walimkosa kosa kumpindua mara mbili. 1964 na 1982. Ila hakufanya malipizi mabaya hivyo.

Aliwakamata akawaweka kizuizini hatimaye aliwaachia. Akina Maganga, Hans Pope, Lugangila nk.

Sheria zilizotungwa kuwalinda watawala zinawaruhusu kufanya lolote bila kushitakiwa hata uchaguzi ukichezewa vipi. Ingeishia tu hapo jamani.
 
Mchuma janga hula na wa kwao! Msemo wa siku nyingi sana huu.

Polepole ameanza kuwa Mtu wa Mungu baada ya kugundua
1. Ubalozi hautorudi tena na hata ukiisha hakutokuwa na uteuzi mwingine wa kumpa leverage aliyokuwa anaitegemea.

2. Baada ya washirika wake wa karibu hususan wale waliokuwa na ndoto za 2030 kufyekwa huko chamana na hawa ni wale waliokuwa wamejiapiza kwamba Samia hakupaswa na asingeweza kuongoza nchi yetu baada ya ule Msiba. Tunamshukuru General Mabeyo na JWTZ kwa kusimamia katiba ya nchi yetu.

3. Amekuwa Mtu wa Mungu na amezaliwa baada ya Rais Samia kutwaa Madaraka kabla ya hapo alikuwa mbinguni na hakuona wala kusikia utekaji na mauaji yaliyokuwa yakifanyika wakati ule yeye akiwa Mwenezi wa CCM na baadae Mbunge wa kuteuliwa. Hakuona kabisa kutekwa na kupotea kwa
1. Kanguye
2. Ben Saa Nane
3. Mo Dewji
4. Azory Gwanda
5. Daniel John na wengine wengi

4. Hakuwepo wakati Lissu anapigwa risasi, Lema, Wenje na wengine wanakimbila uhamishoni? Je aliwahi hata kwenda kumpa salamu ya pole Lissu wakati ule. Sio yeye alikuwa Mwenezi wakati hata suala la kuendesha maombi ya kumuombea Lissu linapigwa marufuku. Alifanya nini?

Ni vyema watu wakafahamu kwamba Polepole na kundi lake tunaowaona sasa wanatoka na kuanza kupiga kelele hawafanyi hivyo kwa sababu wanataka haki bali ni kwa kuwa wameingiwa na hofu ya kukosa madaraka na uhakika wa kumuweka Mtu wao kuwa Rais wa nchi 2030.

Hakuleta hizi drama zote wakati ule kwa sababu uhakika wa kula na kutawala ulikuwepo. Kimsingi inampasa akae kimya maana hiki kinachoendelea ni legacy yake yeye na Baba yao. Huyu ni nyoka waliyemtotoa anawatemea sumu. Asihangaike kutaka kuuhadaa umma kana kwamba ni msafi na kuna kitu kipya anaweza kuleta.
 
Back
Top Bottom