Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

29365860_2333482229999515_4995182915475023041_n.jpg

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
 
Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba ila kwa sababu ya njaa na kiu ya mafanikio binafsi ndio huwafanya watu kuubeba japo dhamira zao zikiwa zinawashtaki

Kwahiyo Zitto kutorudi bungeni ndio Tanzania ya viwanda itafanikiwa!

Kweli ccm imekosa kabisa uhalali wa kuendelea kuongoza serikali, kama taifa tunahitaji kuona mipango na sera mbalimbali zenye tija na uelekeo wa kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati, na siyo blah blah za kijinga zisizo na afya kwa ustawi wa nchi hii

Tunahitaji kuona mfumo wa uboreshaji wa elimu bure, kilimo chenye tija kinachoendana na mazingira ya sasa na siyo kilimo cha kutegemea matone ya mvua kutoka mawinguni, uchumi kuimarika badala ya kudorora, huduma bora za afya n.k

Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli

Mmeshindwa kupambana na changamoto za wananchi mmeamua kuyafanya mawazo mbadala kama ni tatizo nchi hii! Sijui nani aliwaambia kama sisi kipaumbele chetu kama taifa ni kuua upinzani wa vyama! Upinzani hatuna tatizo nao kabisa, tatizo ni ninyi kushindwa kuwa sehemu ya viongozi na kujigeuza kuwa watawala.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Hivi hiyo miradi ni pesa za CCM au pesa za walipakodi??? Sasa kivp CCM wanaruhusiwa kukagua miradi ila zitto akienda kwenye miradi inayotekelezwa na madiwani wa kata zilizo chini ya ACT wanazuiwa???

Polepole anachofanya ni siasa ila nashangaa wapinzani wanaambiwa siasa mpala 2020!! Kujipigia kampeni kama hivyo ni siasa tosha sasa sielewi walichozuia ni kipi???

Hizo ni pesa za walipakodi hivyo mradi ni wa umma sio wa chama flani cha siasa kiasi wakitumie kama kampeni ya 2020!!!

Ajifunze kwa nape leo ngoja ajipendekeze mwisho wake utafika tu
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa alafu cha kuchekesha jimbo hilo limeshawahi kuwa chini ya CCM kwa takriban miaka 40 na hakuna la maana wabunge wa CCM walifanya leo hii wanataka kulirudisha kwa hoja gani??

Yaani wanataka kurudisha majimbo yote ya upinzani CCM kana kwamba majimbo yaliyo chini ya CCM kwa miaka 60 kama chemba, uyui au kibakwe yana maendeleo makubwa hadi kutuaminisha jimbo likirudi ccm linapata maendeleo!!

Hawa jamaa wanashangaza sana
 
Bora mr.porepore chapa kazi uzibe ombwe la waziri wa maji maana hii wizara haujulikani kama ina waziri au la!!
 
Wananchi ndio wanaomchagua wanayemtaka awaongoze, kazi ya CCM ni kubaka matakwa ya wananchi ya kumchagua mtu wanaye mtaka awaongoze na kumtakangaza mtu ambaye hakuchaguliwa na wananchi na kuwalazimisha wananchi wakubali kuongozwa na mtu ambaye hawakumchagua kwa kutumia mtutu wa bunduki hata Kama hawapendi lazima wakubali wapende wasipende.

Labda Kama Polepole alikuwa anamaanisha hivyo ndio Zitto atatafuta kazi ya kufanya kwa kuwa haki ya wananchi ya kumchagua mtu wanayemtaka awaongoze itabakwa na CCM na kumtangaza mtu ambaye hakuchaguliwa na wananchi huku wananchi wakilazimishwa kumkubali chini ya mtutu wa bunduki.

Lakini Kama haki ingekuwa inatendeka, maamuzi ya wananchi yangekuwa yanaheshimiwa, Zitto pamoja na wapinzani wengine wangendelea kuwepo/wataendelea kuwepo kwenye nafasi zao Kama kawaida.
 
Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba ila kwa sababu ya njaa na kiu ya mafanikio binafsi ndio huwafanya watu kuubeba japo dhamira zao zikiwa zinawashtaki

Kwahiyo Zitto kutorudi bungeni ndio Tanzania ya viwanda itafanikiwa!

Kweli ccm imekosa kabisa uhalali wa kuendelea kuongoza serikali, kama taifa tunahitaji kuona mipango na sera mbalimbali zenye tija na uelekeo wa kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati, na siyo blah blah za kijinga zisizo na afya kwa ustawi wa nchi hii

Tunahitaji kuona mfumo wa uboreshaji wa elimu bure, kilimo chenye tija kinachoendana na mazingira ya sasa na siyo kilimo cha kutegemea matone ya mvua kutoka mawinguni, uchumi kuimarika badala ya kudorora, huduma bora za afya n.k

Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli

Mmeshindwa kupambana na changamoto za wananchi mmeamua kuyafanya mawazo mbadala kama ni tatizo nchi hii! Sijui nani aliwaambia kama sisi kipaumbele chetu kama taifa ni kuua upinzani wa vyama! Upinzani hatuna tatizo nao kabisa, tatizo ni ninyi kushindwa kuwa sehemu ya viongozi na kujigeuza kuwa watawala.
Lakini mkuu ukumbuke kuwa Polepole hakulihutubia taifa kutokea Kigoma,bali alizungumza na wana kigoma namna ya kuzikabili changamoto za hapo. Wakati Kigoma ikipatiwa Maji safi na salama, taifa linashughulikia mambo makubwa yenye sura ya kitaifa kama uliyoyaorodhesha hapo na mengine yanayoendelea.
 
Hivi hiyo miradi ni pesa za CCM au pesa za walipakodi??? Sasa kivp CCM wanaruhusiwa kukagua miradi ila zitto akienda kwenye miradi inayotekelezwa na madiwani wa kata zilizo chini ya ACT wanazuiwa???

Polepole anachofanya ni siasa ila nashangaa wapinzani wanaambiwa siasa mpala 2020!! Kujipigia kampeni kama hivyo ni siasa tosha sasa sielewi walichozuia ni kipi???

Hizo ni pesa za walipakodi hivyo mradi ni wa umma sio wa chama flani cha siasa kiasi wakitumie kama kampeni ya 2020!!!

Ajifunze kwa nape leo ngoja ajipendekeze mwisho wake utafika tu
Mkuu tunatatizo kubwa sana katika awamu hii ya 5, viongozi hawana uwajibikaji wa pamoja na kibaya zaidi hakuna priorities
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV

Hii ni kweli kabisa. Nitafanya kazi ya Urais
 
Kasi ya rais magufuli itafagia upinzani uchwara wengi 2020.
na kweli kwa kupachika makada wa ccm kama wasimamizi, kuwanyima viapo kama mlivyofanya uchaguzi wa madiwani, kuwafukuza kwenye vyumba vya kuhesabia kura mubaki wenyewe mbadilishe matokea, kuiba mabox ya kura na kurudishwa yakiwa yana kura tayari, hapo sawa mtashinda kwa kishindo tu
 
Hicho kijamaa bana,hata sikaelewagi.kazi kuchongachonga tu
 
Back
Top Bottom