Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Mkuu umeongea ukweli kabisa alafu cha kuchekesha jimbo hilo limeshawahi kuwa chini ya CCM kwa takriban miaka 40 na hakuna la maana wabunge wa CCM walifanya leo hii wanataka kulirudisha kwa hoja gani??

Yaani wanataka kurudisha majimbo yote ya upinzani CCM kana kwamba majimbo yaliyo chini ya CCM kwa miaka 60 kama chemba, uyui au kibakwe yana maendeleo makubwa hadi kutuaminisha jimbo likirudi ccm linapata maendeleo!!

Hawa jamaa wanashangaza sana
Ccm ina survive kwa sababu ya ujinga, umasikini na maradhi ya Watanzania, huwezi kuwa na taifa lililostaarabika ukakumbatia chama kilichoshindwa kutatua changamoto za miaka nenda rudi.

Ndio maana kwa sasa hawana ushawishi wa hoja zaidi ya kutisha, kujeruhi kuua na kuvunja katiba na sheria za nchi waziwazi tofauti na awamu zilizopita
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
Polepole ww ni Mteuliwa kabla kutoa kauli itadhimini kwanza. Zitto ni Mchumi kwa hiyo hawezi kuangaika hata uhadhuri ni kazi kwani huko vyuoni kuna watu hawajapata elimu ya uraia kwa hiyo atakuwa sio zitto wa mchezomchezo .Unamkumbuka Chachagechage na wengine wengi kwa hiyo kaa nalo hili
 
Hii ni kweli kabisa. Nitafanya kazi ya Urais
Naona povu limeanza...Kama hautaachana na twitter na kujikita kwenye issue za wana kigoma ni wazi ubunge ni bye bye....
 
inajulikana 2020 hakuna upinzani atakaerudi bungeni sijui kama mbowe na wenzake wanalitambua hilo. ccm itachukua majimbo yote kwa nguvu na hili ni agizo kila mkurugenzi wa halmashauri analijua.
 
Kama Polepole anakagua miradi inayotekelezwa na serekali ya CCM haulizwi wala haambiwa Kuwa kufanya hivyoni kosa kwa Kuwa mikutano ya wanasiasa na kazi zozote za wanasiasa zimepigwa marufuku kufanywa tofauti na majimboni kwao.

Wakati huohuo Zitto ambaye maneno haya yamesemewa jimboni kwake ana kamatwa na kuswekwa lupango Kwa Kuwa amekwenda kugua miradi inayosimamiwa na madiwani wa chama chake. Kwa ubaguzi Kama huu kweli Mungu atakwenda kutupa nafasi ya kuwaongoza malaika Kama tulivyoomba?.
 
Kama Polepole anakagua miradi inayotekelezwa na serekali ya CCM haulizwi wala haambiwa Kuwa kufanya hivyoni kosa kwa Kuwa mikutano ya wanasiasa na kazi zozote za wanasiasa zimepigwa marufuku kufanywa tofauti na majimbo yao.

Wakati huohuo Zitto ambaye maneno haya yamesemewa jimboni ana kamatwa na kuswekwa lupango Kwa Kuwa amekwenda kuguwa miradi inayosimamiwa na madiwani wa chama chake Kwa ubaguzi Kama huu kweli Mungu atakwenda kutupa nafasi ya kuwaongoza malaika Kama tulivyoomba?.
Taifa limekosa dira mkuu, ni mwendo wa kuvunja miiko ya taifa hili kwa kukanyaga katiba na sheria zake
 
Back
Top Bottom