Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba ila kwa sababu ya njaa na kiu ya mafanikio binafsi ndio huwafanya watu kuubeba japo dhamira zao zikiwa zinawashtaki

Kwahiyo Zitto kutorudi bungeni ndio Tanzania ya viwanda itafanikiwa!

Kweli ccm imekosa kabisa uhalali wa kuendelea kuongoza serikali, kama taifa tunahitaji kuona mipango na sera mbalimbali zenye tija na uelekeo wa kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati, na siyo blah blah za kijinga zisizo na afya kwa ustawi wa nchi hii

Tunahitaji kuona mfumo wa uboreshaji wa elimu bure, kilimo chenye tija kinachoendana na mazingira ya sasa na siyo kilimo cha kutegemea matone ya mvua kutoka mawinguni, uchumi kuimarika badala ya kudorora, huduma bora za afya n.k

Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli

Mmeshindwa kupambana na changamoto za wananchi mmeamua kuyafanya mawazo mbadala kama ni tatizo nchi hii! Sijui nani aliwaambia kama sisi kipaumbele chetu kama taifa ni kuua upinzani wa vyama! Upinzani hatuna tatizo nao kabisa, tatizo ni ninyi kushindwa kuwa sehemu ya viongozi na kujigeuza kuwa watawala.

CC: Elitwege
 
Tulia usome kwa umakini uelewe si kukimbilia kujibu
Polepole anakagua miradi kama nani?? Kwani CCM ndio inatoa pesa za miradi hadi atishie kwamba zitto harudi 2020??

Angekuwa waziri au mbunge wa CCM well and good ila sio mwanasiasa wa CCM ambaye hayupo serikalini alafu anatoa maagizo tu kana kwamba mradi umetoka kwa hela za chama chake while ni pesa za walipakodi hata wasio na vyama

Alafu kituko madiwani wa Upinzani wanakatazwa kukagua miradi waliopitisha kwenye halmashauri zao ila CCM tena mtu asiyekiongozi wa serikali anakagua na kutoa maagizo

Polepole ajifunze kwa nape, alijikomba zaidi yake ila leo hii kapotezewa.... Haya jua linazama hivyo
 
......miradi inayotekelezwa na madiwani wa kata zilizo chini ya ACT.....
Hao madiwani wanatekeleza ilani ya ccm maana ndiyo iliyoshinda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Ilani za vyama vingine zilishindwa, hivyo haviwezi na hairuhusiwi kisheria kutekelezwa sehemu ye yote ya nchi. Hii ni kwa mjibu wa katiba na sheria zetu. Ilani ya ccm inatekelezwa nchi nzima. Jimbo la ushindi la ccm ni nchi nzima na ndiyo maana Polepole ana legacy ya kutembea nchi nzima na kukutana na wananchi popote pale nchini kuhamasisha, kuelimisha na kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo ya nchi.
 
Mh Rais mwenyewe alitoa mwisho Iwe mwezi wa 11 mwaka jana(2017)
Yy nani Mr Buyer Slow slow!??[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Hawa jamaa kila mtu anaongea lake kutegemeana na ameamkaje. Halafu wanafanya kazi kwa style ya Mungu wakati wa uumbaji ambaye alikuwa anaamrisha kwamba "Na iwe bahari"- inakuwa, "Na iwe nchi"-inakuwa!

Kuna watu walitaka kumfikia Mungu mbinguni kwa kujenga Mnara wa babeli. Ikabidi Mungu awachanganye wasielewane katika lugha, na hatimaye hawakufanikisha lengo lao. Kwa hawa jamaa, nawaachia msemo mmoja kwamba 'A dying Horse has strong kicks'!

Wakipata muda watatafakari!
 
Hao madiwani wanatekeleza ilani ya ccm maana ndiyo iliyoshinda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Ilani za vyama vingine zilishindwa, hivyo haviwezi na hairuhusiwi kisheria kutekelezwa sehemu ye yote ya nchi. Hii ni kwa mjibu wa katiba na sheria zetu. Ilani ya ccm inatekelezwa nchi nzima. Jimbo la ushindi la ccm ni nchi nzima na ndiyo maana Polepole ana legacy ya kutembea nchi nzima na kukutana na wananchi popote pale nchini kuhamasisha, kuelimisha na kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo ya nchi.
Embu usitufanye wote hatujui sheria... Kama ilani ikipitishwa si inazaa mpango wa taifa wa miaka 5 ambao unakuwa hauna CHAMA ila wa WATANZANIA wote na ilani ya CCM inageuka illani ya KITAIFA sasa hayo ya kusema ilani ya CCM ndio kisheria inatakiwa kutekelezwa umeutoa wapi?? Mara 10 ungesema mpango wa taifa hapo sawa ila ilani ya CCM inaukomo hapo

Pia unaposema kila mradi ni wa ilani ya CCM ina maana kwa mfano Meya jacob alikuta wamama wanalialia maisha magumu wote tulishuhudia alitoa mikopo kma meya wa wa ubungo kwa vikundi kadhaa vya wanawake je hapo imetekelezwa ilani ya CCM au ina maana gani sasa upinzani kuongoza halmashauri kma hawawezi tekeleza sera zao??? Unapotosha kwa faida ya nani

Jimbo la ushindi la CCM ni nchi nzima kasema nani?? CCM inashika serikali tu sasa jimbo ni nchi nzima una maana polepole anaweza kwenda mahakama kuu kutoa maagizo na yakatekelezwa kisheria ?? Embu acheni kurasimisha uhuni wenu CCM inaposhinda inapewa mamlaka juu ya serikali hivyo mambo yote ya utekelezaji wa sera unafanywa na serikali maana ukishashika utawala uchama unakufa hapo ndio maana watendaji wa serikali huwa hawashauriwi kuwa na mrengo wa kisiasa!!! Sasa toka lini mwanaCCM asiye na cheo serikalini akatoa maagizo kwa vyombo vya serikali na vinatiii?? Nipe kifungu hapa kwenye sheria yoyote inayokubaliana na upuuzi huu

Kama polepole anataka apewe wizara serikalini sio katibu mwenezi kugeuka kiongozi wa serikali huu ni upuuzi hata sijui hiyo PhD yako umeipataje kama unasupport mambo ya kihuni namna hii
 
Pole pole nae ajue ukatibu uenezi wake una mwisho wake ajue cheo ni dhamana.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
Aah kumbe Chakubanga!atajibiwa na Bulicheka
 
Ukiona mwanaume mtu mzima lakini ngozi yake ya usoni imegoma kuotesha ndevu basi ujue ana kasoro kubwa sana kichwani haswa kwenye upande wa fikra za kiume. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Pole pole hana ndevu.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
Kwani ubunge ni ajira?!!!
 
Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba ila kwa sababu ya njaa na kiu ya mafanikio binafsi ndio huwafanya watu kuubeba japo dhamira zao zikiwa zinawashtaki

Kwahiyo Zitto kutorudi bungeni ndio Tanzania ya viwanda itafanikiwa!

Kweli ccm imekosa kabisa uhalali wa kuendelea kuongoza serikali, kama taifa tunahitaji kuona mipango na sera mbalimbali zenye tija na uelekeo wa kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati, na siyo blah blah za kijinga zisizo na afya kwa ustawi wa nchi hii

Tunahitaji kuona mfumo wa uboreshaji wa elimu bure, kilimo chenye tija kinachoendana na mazingira ya sasa na siyo kilimo cha kutegemea matone ya mvua kutoka mawinguni, uchumi kuimarika badala ya kudorora, huduma bora za afya n.k

Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli

Mmeshindwa kupambana na changamoto za wananchi mmeamua kuyafanya mawazo mbadala kama ni tatizo nchi hii! Sijui nani aliwaambia kama sisi kipaumbele chetu kama taifa ni kuua upinzani wa vyama! Upinzani hatuna tatizo nao kabisa, tatizo ni ninyi kushindwa kuwa sehemu ya viongozi na kujigeuza kuwa watawala.
Well said mkuu
 
Wabunge wenye midomo lazima kura zao ziporwe wanauhakika 100% watazipora na hatarudi kama siyo kuzipora wanajuaje maamuzi ya wapiga kura
 
Anapiga kampeni huyo, double standard.
 
Back
Top Bottom