Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba ila kwa sababu ya njaa na kiu ya mafanikio binafsi ndio huwafanya watu kuubeba japo dhamira zao zikiwa zinawashtaki

Kwahiyo Zitto kutorudi bungeni ndio Tanzania ya viwanda itafanikiwa!

Kweli ccm imekosa kabisa uhalali wa kuendelea kuongoza serikali, kama taifa tunahitaji kuona mipango na sera mbalimbali zenye tija na uelekeo wa kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati, na siyo blah blah za kijinga zisizo na afya kwa ustawi wa nchi hii

Tunahitaji kuona mfumo wa uboreshaji wa elimu bure, kilimo chenye tija kinachoendana na mazingira ya sasa na siyo kilimo cha kutegemea matone ya mvua kutoka mawinguni, uchumi kuimarika badala ya kudorora, huduma bora za afya n.k

Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli

Mmeshindwa kupambana na changamoto za wananchi mmeamua kuyafanya mawazo mbadala kama ni tatizo nchi hii! Sijui nani aliwaambia kama sisi kipaumbele chetu kama taifa ni kuua upinzani wa vyama! Upinzani hatuna tatizo nao kabisa, tatizo ni ninyi kushindwa kuwa sehemu ya viongozi na kujigeuza kuwa watawala.
Huyu bwana slowslow anamuogopa sana mkulu ndo mana anafanya ujinga anaopenda mkulu.
 
Hivi anachofanya polepole sio siasa? Maana siasa zimezuiwa hadi 2020!!!
 
Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli
Hivi una anzia wapi kuwaamin baadhi kuwa siyo maadui wanapofikia kuitaka jumuiya ya kimataifa ituwekee vikwazo vya kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kadhalika....unaanzia wapi kuwaamini baadhi wanapoamua kwenda nchi ya jirani na kutumia vyombo vya nchi hiyo kuisema vibaya serikali ya nchini mwao...unaaazia wapi, na kuuliza.
===
Upinzani kuna baadhi ya watu muhimu sana wanaoitakia mema nchi yetu lakini wanazimwa na hawa ambao wanatupa mashaka ya uaminifu wao kwa nchi kwa maneno yao na matendo yao na wana sauti kweli hawa.
 
Sio Zitto tuu

Tunajua agenda yenu ccm ya kutumia vyombo vya usalama ili kuua upinzani wote

Ndio maana tunataka kukomesha huu upumbavu ifikapo 26/4/2018
 
kwani slow slow ana kura ngapi atakazopiga huko kigoma?
 
POLEPOLE usijidanganye ccm inachukiwa na ndio Maana anatumia nguvu kushinda
 
2020 polepole ajiandae atuachie chama chetu tumemchoka ebo
 
[emoji53][emoji53][emoji53]
IMG_20180307_17862.jpg
 
Zitto atakoma kuwa mbunge ikiwa tu wale wazee wa pale Kigoma watakapo sema hawamhitaji kwa sasa,lakini sio kwa kauri ya Pole pole
 
Kasi ya rais magufuli itafagia upinzani uchwara wengi 2020.
Kasi gani? Kuchukua pesa za Umma, pesa za walipa kodi kuwanunua Wapinzani, kurudia chaguzi? Pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo ni kubwa sana ni pesa ambazo zingeweza kujenga Hosptal za rufaa kila mkoa na kuajiri madaktari toka India na wagonjwa wote wakatibiwa nchini pasipo kupelekwa nje,
 
Mabilioni anayovuna kwenye huu mradi haramu wa kununua wapinzani uchwara yamempa kiburi sana huyu chakubanga.
Mladi wa ununuzi wapinzani, kurudia uchaguzi, Uchakachuaji,wizi wa kura, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi akina Lisu, kuwafunga jela akina Sugu ni mladi haramu wa pesa za walipa kodi lakini Madalali wa siasa huko CCM wameneemeka mpaka wamejitoa fahamu kwa kiwango cha kutisha
 
Kweli kasi ya kuteka na kupiga watu risasi, kununua wapinzani ni aibu kwa ccm
Kibaya wanakula pesa za Umma, pesa za walipa kodi ambao ni watanzania wote, Wageni toka nje na watu wasio na vyama, pesa zao zinachukuliwa Hazina kienyeji na kutumika kwa mambo ya hovyo hovyo tu, ni Ufisadi na ufujaji wa pesa za Umma kwa kazi haramu za kienyeji zisizo na tija wala kujulikana.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
PolePole hajakosea kwa sababu ubunge wa Zitto wa 2015 ulifanikishwa na CCM. Bila maagizo ya ccm Zitto alikuwa ameshaanguka ubunge Kigoma mjini. Akamuulize Kafulila kwa sababu hayo ndio yafuatayo Kigoma Mjini 2020.
 
Back
Top Bottom