Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

nyuso zingine ndio maana huwezi jua kama zina ukoma au hazijanwa majihazina soni.
 
Na yy atafute kaz nyingine.Hii ya sasa imemshinda.kaz ya ununuzi na ugavi wa wanasiasa sio nzuri..
 
na kweli kwa kupachika makada wa ccm kama wasimamizi, kuwanyima viapo kama mlivyofanya uchaguzi wa madiwani, kuwafukuza kwenye vyumba vya kuhesabia kura mubaki wenyewe mbadilishe matokea, kuiba mabox ya kura na kurudishwa yakiwa yana kura tayari, hapo sawa mtashinda kwa kishindo tu

Ili kuokoa pesa watangeze tu majimbo yaliyowazi including la zitto wateu watu wao hiyo pesa tukachimbie visima kule tarura ya maji.
 
Sijui polepole anaongea na injinia wa maji kama nani...hii nchi ni ya maajabu
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV

Kazi ya usambazaji wa maji either ni ya wizara ya maji na umwagiliaji au halmashauri ya mji
Katibu mwenezi anaweza kusubiri miradi ikishafunguliwa awaambie wananchi jinsi serikali ilivyoweza kutimiza ahadi zake
Kumpangia mkandarasi targets hiyo ni kazi ya wizara, mhandishi wa maji, au mkurugenzi
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

View attachment 718311

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Chanzo: EATV
Zito ni msomi mzuri tuu. Ana karata nyingi ikiwemo ya kuhamia kwenye chama dola. 2020 wapinzani watahamia wote CCM hata wao wanahitaji kula na wanafamilia pia
 
Hii zana ya kununua ni kichaka kipya cha ufipa boys kujificha ili wapate nafuu wakati chama kinateketea.

Stop this nonsense .
Mungu aliongea nasi kwa kupitia mbunge Nasari akafanya kazi kiusahihi kama alivyotumwa na iliyompendeza Mungu kuleta ushahidi wa kununua madiwani ( Mnyeti). Sio lazima ukubali lakini ukikataa huu ushahidi wewe utakuwa shetani. Boy stop satanic behavior!!!!
 
Back
Top Bottom