tamuuuuu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 21,329
- 28,063
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Oh! Kwa hiyo successes na failures za utekelezaji wa masuala ya maendeleo kwenye majimbo na kata zote ni matunda ya CCM, siyo? Natumaini mtakumbuka hili kwenye kampeni, na siyo muanze kuwaponda wapinzani kwa kushindwa 'kuleta' maendeleo kwenye majimbo na kata zao.Hao madiwani wanatekeleza ilani ya ccm maana ndiyo iliyoshinda kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Ilani za vyama vingine zilishindwa, hivyo haviwezi na hairuhusiwi kisheria kutekelezwa sehemu ye yote ya nchi. Hii ni kwa mjibu wa katiba na sheria zetu. Ilani ya ccm inatekelezwa nchi nzima. Jimbo la ushindi la ccm ni nchi nzima na ndiyo maana Polepole ana legacy ya kutembea nchi nzima na kukutana na wananchi popote pale nchini kuhamasisha, kuelimisha na kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo ya nchi.
Anadhani Kigoma kuna malofa wapumbavu.Mh Rais mwenyewe alitoa mwisho Iwe mwezi wa 11 mwaka jana(2017)
Yy nani Mr Buyer Slow slow!??[emoji1] [emoji1] [emoji1]
Mkuu jina maarufu wanaitwa "MALOFA WAPUMBAVU"Mkuu umeongea ukweli kabisa alafu cha kuchekesha jimbo hilo limeshawahi kuwa chini ya CCM kwa takriban miaka 40 na hakuna la maana wabunge wa CCM walifanya leo hii wanataka kulirudisha kwa hoja gani??
Yaani wanataka kurudisha majimbo yote ya upinzani CCM kana kwamba majimbo yaliyo chini ya CCM kwa miaka 60 kama chemba, uyui au kibakwe yana maendeleo makubwa hadi kutuaminisha jimbo likirudi ccm linapata maendeleo!!
Hawa jamaa wanashangaza sana
Anamhamisha yeye? Afanye kilichompa kitiKatibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)
View attachment 718311
Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.
"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020
Chanzo: EATV