Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Hapa chini nimeattach barua ya mwana kijiji mmoja wa huko kigoma ambaye alibambikiwa kesi na polisi ,akaifikisha kesi kwa mkuu wa wilaya hiyo Kibondo mkoani Kigoma bwana Venance Mwamoto,lakini mpaka leo akaingiza siasa kwenye hilo jambo,
Naomba Moderator mmnisaidie kuiweka vizuri kwa sababu mimi sio mtaalamu sana wa hizi technologia za ng'ambo
A%20S%20576.gif
 

Attachments

plz mods nisaidieni kuiweka vizuri hii attachment,mnisaidie kuifungua ili wenye kutumia simu waweze kuisoma nao huku wakiiona vizuri
A%20S%20576.gif
 
fungua attachment ujionee mwenyewe hali halisi....................
 
weka picha ya shehe ponda,bomu la arusha....pls
 
hali ni tete sana kwa taifa langu Tanzania Mungu turehemu na haya maswaiba
 
Ripoti hiyo iliyoambatanishwa ambayo ni ya kichochezi iliyoandikwa kwa nia ya kuizuia marekani na nchi za magharibi kuipa misaada Tanzania ina makosa mengi hasa ya kuangalia upande mmoja yena wa mrengo wa kichama zaidi. Pamoja na hayo mengi ni ya kusadikika hakuna ushahidi wa moja kwa moja mfano hlisi ni hamna barua iliyoandokwa na Kikwete kuidhinisha mpango wa Irani, hakuna barua toka Irani kwa Kikwete, Kikwete kama Rais lazima akutane na wawakilishi wa mataifa mbalimbali ikiwemo Irani na nchi nyingine unazodhani ni mbaya kwa kuwa tu Marekani haishirikiani nayo.

Kumbuka Tanzania haifungamani na upande wowote. Kumbuka Marekani inayopewa muongozo na wanaojiita wenye haki za binadamu ina uwezo mkubwa wa kuchunguza mambo kuliko tunavyodhani lakini ndiyo haohao marais wake wanaingia humu nchini na wafanyabiashara zao. Kumbuka hamna nchi duniani yenye uwezo wa kuacha watu wachache waharibu amani au usalama wa nchi nzima kwa kuhofia haki za binadamu Drones zinafanya kazi gani Iraq, Afganistan na kwingineko?

Kama kweli hao jamaa wana issues za ukweli na siyo kwamba wanajikomba kupata misaada ili wajenge majumba yao na kununua magari ya kifahari basi waiandikie congress iunde tume maalumu isiyofungamana na upande wowote ifanye uchunguzi wa kina kwa serikali na mashirika yanayojiita yasiyo ya kupata faida (NPOs) kuona serikali inavyotimiza wajibu wake na mashirika hayo yanavyotimiza wajibu wake. Maana mwisho wa siku tutakua kama dafur ambayo imeharibiwa na NGOs/NPOs hasa za magharibi ambazo hukusanya pesa nyingi kutoka kutoka ulaya na kimsingi hawako tayari kuona amani ikirejea. Mfano mwingine ni mashirika ya wakimbizi au yanayoshughulikia UKIMWI unadhani yako tayari vita au ukimwi uishe la hasha ajira nayo iishe haiwezekani.

Mwisho sioni sababu ya kuishadadia hii ripoti labda tu kuvuta hisia ili kupata umaarufu wa kisiasa lakini baada ya kushinda kwenye uchaguzi kazi ni ileile hakuna serikali inayokubaliwa 100% na wananchi wake.
 

Like Sabibo Camp like Operesheni Tokomeza. Na hii ni just a drop of ice berg...unaweza kupata wakati mgumu kujiuliza kwa nini hadi sasa serikali haijawajibika kikamilifu katika unyama huu waliofanyiwa Watanzania.

Hivi unaweza kujiuliza kwenye hizo kambi vingapi hatujavijua vilifanyika? Kama hadi sasa, kwa mujibu wa Tundu Lissu akihutubia mkutano wa Shelui na Gervas Mbasa akihutubia Nanga, wapo watu tena akina mama walipigwa misumari ya nchi sita masikioni, wanaume walilazimishwa kufanya mapenzi na miti hadi wamalize haja zao, wengine wakatiwa chupa na misumari sehemu za siri. OMG! Mangapi hatuyajui!

Shameful condition...but they should know exactly, no condition is permanent (The State of Africa; A History of Fifty Years of Independence [Martin Meredith].
 
Sasa kichura na viboko si mambo ya kawaida huko jeshini. Kwao ni sehemu ya mafunzo ya ukakamavu na uvumilivu.

Kiongozi wa N.korea kamua mjomba wake na watu wanaomuunga mkono kwa kutumia antiaircraft machine gun hapo watu wa haki za binadamu mnasemaje?
 
Kama Mwangosi aliuwawa kikatili zaidi na video zikaonyesha lakini bado wahalifu wanadunda mtaani na wengine kupandishwa vyeo,hata hii nayo itapuuziwa tu na hawa watawala "mchwara"
 
Back
Top Bottom