Police militarization ni mchakato wa taasisi za polisi kuanza kufanana na jeshi kwa kutumia vifaa vya kivita, mbinu za kijeshi, na mienendo ya ukakamavu uliopitiliza katika kushughulikia masuala ya kiraia. Hali hii imezua mijadala duniani kuhusu usalama, haki za binadamu, na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Tanzania, kama nchi nyingine nyingi barani Afrika, imewahi kushuhudia matukio ambayo polisi wanatajwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, na hivyo kuzua hoja juu ya kiwango cha “umilitari” ndani ya polisi.
Matukio ya nchi nyingi yanaonyesha kuwa polisi wanapokuwa “wamemilitarishwa,” uwezekano wa kutumia nguvu kali katika maandamano huongezeka. Kisaikolojia, mafunzo na vifaa vya kijeshi hutengeneza mazingira ambapo askari anahisi yuko vitani — na si kwenye jamii anayopaswa kuitumikia.
Kwa Tanzania, ripoti mbalimbali zimehusisha matukio ya mauaji ya waandamanaji na:
Dalili za kuonyesha militarization ya polisi nchini ni :
Huu ni mfano wa muonekano Polisi wa Tanzania miaka ya sasa....
Police militarization inamaanisha kuwa kwa polisi wana silaha nzito, ndani ya taasisi ya polisi, na hayan ni mabadiliko yanayojenga taswira ya polisi kama kikosi cha vita badala ya chombo cha kulinda raia.
Tuliozaliwa miaka ya zamani, nguo za polisi zilikuwa ni shati na suruali za khaki zenye utanashati wa kuwa kuonyesha kuwa taswira isiogopesha kwa wananchi kuliko kuwa katika aina ya mavazi yenye vinasaba vya uanajeshi
Na pia silaha walizoaminiwa kutulinda zilishabihiana na kazi zao...
Kwa miaka kadhaa, mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyombo vya habari yameripoti matukio ambapo polisi nchini Tanzania walitajwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano au mikusanyiko ya kisiasa. Katika matukio kadhaa yaliyotajwa, waandamanaji walijeruhiwa au hata kupoteza maisha kutokana na matumizi ya risasi za moto, mabomu ya machozi, au nguvu kupita kiwango.
Ingawa serikali mara nyingi hutetea hatua hizo kwa kusema kuwa ni kulinda usalama na kudhibiti machafuko, hoja kuu inayojitokeza ni iwapo kiwango cha nguvu kilichotumika kilikuwa cha lazima na iwapo mbinu za polisi zilipishana na maadili ya utendaji wa kiraia.
Wakati wa karibu na uchaguzi, kumekuwa na ongezeko la oparesheni za polisi zenye sura ya kijeshi zaidi. Aina hii ya mabadiliko mara nyingi huchochea hofu miongoni mwa wananchi, na huongeza hisia kwamba polisi hawatofautiani sana na majeshi ya ulinzi.
Tanzania ina mfumo ambao polisi ni chombo cha kiraia, wakati jeshi ni chombo cha ulinzi wa mipaka na maslahi ya taifa kwa ujumla. Hata hivyo, mgongano unatokea pale askari polisi kupitia mafunzo ya aina ya kijeshi, hasa wa vikosi maalum kama FFU, na pia kuwa ma matumizi ya silaha nzito zenye uwezo wa kijeshi.
Hii dhamira inaweza kutumiwa na watawala ili kujilinda na hatari ya mapinduzi ya kijeshi, endapo polisi wanaweza kuwa na uwezo wa kukabiliana na jeshi la nchi kwa kuwa na silaha nzito.
Hii huongeza uwezo wa operesheni maalum na pia kuwa na silaha nzito za kijeshi na kuwa na nguvu ya kukabiliana hata majukumu ya jeshi la nchi.

- Matumizi ya risasi za moto katika kudhibiti umati, hali ambayo haikubaliki katika viwango vya kimataifa
- Kutokuwa na uwazi katika uchunguzi wa matukio, hivyo kuongeza hisia za kutokuwepo kwa uwajibikaji
- Upungufu wa mafunzo ya utulivu (de-escalation) yanayofundisha kupunguza mvutano badala ya kuongezea
Dalili za kuonyesha militarization ya polisi nchini ni :
- Matumizi ya magari ya kivita au yenye kinga nzito
- Mavazi, vifaa na silaha za kijeshi
- Mafunzo yanayozingatia mbinu za vita
- Uendeshaji wa oparesheni za polisi kwa mtindo wa kijeshi
- Kauli na misimamo inayoweka mkazo juu ya “kupambana” badala ya “kutumikia jamii”