Polisi: Ajali ya Shilole hajaripotiwa kituo chochote cha polisi mkoani Kigoma

Polisi: Ajali ya Shilole hajaripotiwa kituo chochote cha polisi mkoani Kigoma

lugoda12

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
319
Reaction score
648
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok ikidai Msanii wa muziki Shilole kupata ajali ya gari na kujeruhiwa akiwa safarini akitokea Mkoa Kigoma akielekea Mkoa Dodoma ambayo gari aliyokuwa akitumia kwa safari aina ya Toyota Alphad ambayo namba zake za usajili bado hazijafamika iligonga Ng'ombe eneo la Maragalasi wilayani Uvinza.

Ukweli ni kwamba taarifa hiyo ya ajali hajaripotiwa kituo chochote cha Polisi Mkoa wa Kigoma, hata hivyo tunashauri dereva yeyote anapopata ajali akiwa safarini ambayo imepelekea kifo, majeruhi au uharibifu wa chombo anawajibu wa kutoa taarifa Kituo cha Polisi ili aweze kupata msaada wa matibabu, kuchunguza chanzo cha ajali na kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa mtuhumiwa aliyesababisha ajali.

Endapo tukio hilo la ajali lilitokea tunatoa wito kwa Shilole kufika kituo chochote cha Polisi kuripoti ajali hiyo, ili uchunguzi uzewe kufanyika na hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mtuhumiwa aliyesababisha ajali hiyo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linawataka madereva wa vyombo vya moto mkoani Kigoma kuendelea kutili na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kutokea kutokana na uzembe wa madereva.

Pia Soma: Shilole apata ajali akitoka kushiriki 'Pilau day' Kigoma
FB_IMG_1767505707483.jpg
 
Polisi Tz bhana.

Eti kama ajali hyo imetokea, Shilole afike kituo cha POLISI kutoa taarifa.

Inamaana wao hawana intelligence?
 
Hivi hali ya ng'ombe wetu wapendwa inaendeleaje kwa wale walio karibu na eneo la tukio...
 
Ajali nyingi haziripotiwi. Umegonga ng'ombe mchungaji kakimbia una mambo yako ya haraka, pengine leseni ishaisha muda au huna kabisa, labda gari ya magumashi, bima hola yanini kuanza kusumbuana polisi😂
 
Yaani Polisi bila aibu wanakiri kuwa ajali inaweza kutokea tena katika barabara kuu na wao wasiwe na taarifa mpaka muathirika aende kuripoti.

Kwa wenzetu, ajali ikitokea tu automatically wanakuja Polisi, watu wa Fire na Ambulance.
 
Kigoma bhana, hata mwizi akiiba anatakiwa akatoe taarifa kituo cha polisi
 
Back
Top Bottom