Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu mko salama?
Kumekuwa na matokeo mengi yanatokea hivi karibuni watu wanakamatwa na watu wanaojitambulisha ni polisi mwisho wa siku wanaokotwa wamekufa, polisi wakiambiwa ni wao wamefanya hivyo wanagoma kuwa waliowakamata siyo polisi.
Wakati mwingine huwa inatokea wanaomkamata mtuhumiwa kuwa na nguo za polisi lakini bado polisi watasema hizi siyo zare zetu, hakuna polisi aliyeagizwa kufanya jambo hili. Lakini pia kuna hii mtu anakwambia ni polisi anatoa kale ka badge chap na kukirudisha mfukoni hata hujaona vizuri kuwa ni polisi, na kwa jinsi Watanzania tulivyo waoga na hatujui haki zetu hatuulizi zaidi, na ukiuliza unaweza kula mitama mpaka unakubali kuondoka mwenyewe.
Pia soma: Jua haki yako unapokamatwa na Polisi
Lakini pia kuna wale wapepelezi ambavyo kwa nilivyosikia wao huwa hawavai sare, sasa huyu anaruhusiwa kwenda kumkamata mtu? Kama ndio anatakiwa awaje ili mwananchi atambue huyu ni polisi mpelelezi kweli na siyo muuaji aliyeenda kukatisha maisha yake?
Jambo linaloleta mkanganyiko zaidi ni pale inapotokea mtuhumiwa anagoma kukamatwa na mtu aliyejitambulisha kama polisi lakini hajatoa kitambulisho huwa anachukuliwa kwa nguvu. Chukulia mfano wa kesi ya Robert Mushi, ndugu wa Boniface Jacob, mashuhuda walisema walisema waliokuja walijitambulisha kama polisi lakini hawakuwa na gwanda za polisi, na hata Robert alipojaribu kujitetea hawakusikiliza chochote wakaondoka naye. Polisi walipoulizwa wakasema hakuna polisi walioagizwa kutekelezwa hilo na mwisho wa siku jamaa huyo akaibuka amekufa.
Sasa naomba tupate ufanunuzi hapa, polisi akija kukukamata anatakiwa kuwaje? Na akiwa vipi unatakiwa kujilinda na kugoma kuondoka naye?