Polisi anayeenda kumkamata mwananchi anatakiwa kuwaje? Mwananchi anatakiwa kufanya nini ikiwa amegundua mtu huyo siyo polisi?

Polisi anayeenda kumkamata mwananchi anatakiwa kuwaje? Mwananchi anatakiwa kufanya nini ikiwa amegundua mtu huyo siyo polisi?

Mtu anayekuja kukukamata bila vitambulisho mnige roba
Kuna jamaa alitaka kukamatwa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni askari,kitu alikuwa nacho ni pingu tu sijui alizitoa wapi,alichezea kipigo sana kutoka kwa yule mtuhumiwa wake,mwenyekiti wa mtaa akaamulia na polisi wa kituo walipofika wakambeba maana hawakuwa na taarifa kuwa kuna mtu ni askari na ameingia kwenye eneo lao la kazi,
Hao wanaojiita maaskari wazingatie sheria maana kile kipigo jamaa alichezea na watu walikuwa hawaamulii maana aliingia kwa gia mbaya
 
Wananchi anatakiwa kujulishwa nin kimejiri na anatakiwa kituo gani cha police ili awajulishe ndugu zake
 
Askari kutofuata sheria haimaanishi kuwa watu wakubali na kukaa kimya. Kama umesoma na kuelewa ni kuwa mwanzisha thread anazungumzia hili hili la ubabe ambalo wewe unalisema na kuuliza ni nini kinatakiwa kufanyika. Elimu ni muhimu kwa sababu ndiyo njia ya kuanza kuondoa huu ubabe wa polisi. Kadiri watu wengi wanavyojua haki zao, ndivyo watakavyoshirikiana kuondoa huu ubabe. Au wewe ulitakaje? Kwa kuwa wanatumia nguvu hivyo tukae kimya na kukubali!
Polisi ni mwepesi sana kama hujatenda kosa,na wala hujui tuhuma anazokuletea.

Yaani una kimeo unachokijua kabisa halafu wanakuja unaanza kuomba kitambulisho???
Utaendelea kuona ni wababe milele na hakuna siku utaona wanabadilika.
 
Kuna jamaa alitaka kukamatwa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni askari,kitu alikuwa nacho ni pingu tu sijui alizitoa wapi,alichezea kipigo sana kutoka kwa yule mtuhumiwa wake,mwenyekiti wa mtaa akaamulia na polisi wa kituo walipofika wakambeba maana hawakuwa na taarifa kuwa kuna mtu ni askari na ameingia kwenye eneo lao la kazi,
Hao wanaojiita maaskari wazingatie sheria maana kile kipigo jamaa alichezea na watu walikuwa hawaamulii maana aliingia kwa gia mbaya
Watu wote wawe wanakula ugali mwingi ili kuwapiga polisi wasiofata sheria,ila angalizo,hakikisha ni kweli huyo sio polisi.

Otherways Mungu akutie nguvu.
 
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kukri amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

C&P
Mbona hizo haki ni nyepesi sana kughushiwa na 'wasiojulikana'?

Vibali vyote hivyo kughushiwa ni rahisi sana, labda linalobakia bila najisi ni la kiongozi serikali za mtaa pekee ndiyo linabaki kuwa ni alama ya usalama wa rsia!
 
Polisi ni mwepesi sana kama hujatenda kosa,na wala hujui tuhuma anazokuletea.

Yaani una kimeo unachokijua kabisa halafu wanakuja unaanza kuomba kitambulisho???
Utaendelea kuona ni wababe milele na hakuna siku utaona wanabadilika.
Una akili za kijima sana. Anyway, kutembea nchi nyingine nako kunasaidia maana kama hujabahatika kutoka Bongo utadhani dunia yote iko hivyo.
 
Una akili za kijima sana. Anyway, kutembea nchi nyingine nako kunasaidia maana kama hujabahatika kutoka Bongo utadhani dunia yote iko hivyo.
Si kila kilichoko nje ni bora,hii ni dhana ya washamba baada ya kutoka nje mara moja.
 
Si kila kilichoko nje ni bora,hii ni dhana ya washamba baada ya kutoka nje mara moja.
Nani kasema kila kilicho nje ni bora? Inaonyesha hii nadharia unayo wewe kichwani au unadhani watu wanaotoa mifano ya mambo mazuri yanayotokea kwingine dunia wanayo jambo ambalo siyo! Kuna mambo mengi tu ya kwetu ambayo mimi huwa naona ni mazuri kuliko ya nje.
 
😂😂 kitambulisho au sio,utanyooka ubishi,ushawahipigika na ukasingiziwa unazuia askari kutenda kaz yao?
 
Back
Top Bottom