Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Baada ya kusambaa kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa vijana wawili wanaojulikana kama Wachokonozi, yaani Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo, wametekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha, taarifa mpya zimebainisha kuwa madai hayo si ya kweli.
Soma Pia: Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, kupitia Kamanda wa Polisi Justin Masejo, limethibitisha kuwashikilia vijana hao kwa makosa mbalimbali. Hata hivyo, hakufafanua ni makosa gani na amesema uchunguzi bado unaendelea, na baada ya kukamilika taarifa kamili zitatolewa. Hata hivyo, hakueleza wazi ni katika kituo gani cha polisi vijana hao wanashikiliwa hadi sasa.