Polisi Arusha: Ni kweli tunawashikilia Wachokonozi kwa makosa mbalimbali

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Baada ya kusambaa kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa vijana wawili wanaojulikana kama Wachokonozi, yaani Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo, wametekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha, taarifa mpya zimebainisha kuwa madai hayo si ya kweli.

Soma Pia: Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, kupitia Kamanda wa Polisi Justin Masejo, limethibitisha kuwashikilia vijana hao kwa makosa mbalimbali. Hata hivyo, hakufafanua ni makosa gani na amesema uchunguzi bado unaendelea, na baada ya kukamilika taarifa kamili zitatolewa. Hata hivyo, hakueleza wazi ni katika kituo gani cha polisi vijana hao wanashikiliwa hadi sasa.

Your browser is not able to display this video.

​
 
Hata hivyo, hakufafanua ni makosa gani na amesema uchunguzi bado unaendelea, na baada ya kukamilika taarifa kamili zitatolewa.
"UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA" hii ni kauli ya KIPUMBAVU sana kwa jeshi letu.

Watu mna tools zote za kufanya uchunguzi, kwanini msifanye uchunguzi kabla kisha ndio mkawakamate?

Failed State.
 
Eti taarifa sio za kweli?Kama walikuja na silaha hawajajitambulisha,kwanini wasiitwe watu wasiojulikana? Wameona hali mbaya ndio wanajitokeza
 
Vinginevyo Wangeuawa kama walivyouawa wengine akiwemo Ally Kibao.

Tunawashukuru wote mliopaza sauti zenu na kunusuru vijana hawa kupewa Fisi wa Katavi

 
Jamaa anaongea kama kapangwa,alafu ukiangalia
Hyo video nyuma jamaa mwenye kapelo sjui a angalia viatu,mbona simuelewi elewi

Ova
 
Piga mafala hao , miongoni mwa vijana wajinga na mitumba yao huko Arusha ..Chapa kabisa wanapotosha Umma.

Safi sana serikali kukamata hawa kenge,tena washamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…