Maafisa wa Jeshi la Polisi wamefika mapema hii leo katika msiba wa kijana Sefu Mussa, mkazi wa Matejoo jijini Arusha, ambaye alifariki dunia baada ya kudaiwa kupewa adhabu na askari watatu wa Hifadhi ya Ngorongoro.
Sefu anadaiwa kufariki baada ya yeye na wenzake kupotea njia tarehe 12 Aprili 2026, wakati wakielekea kwenye mazishi ya rafiki yao huko Babati, na badala yake kuingia katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambako walikutana na askari hao.
Soma pia:Askari watatu wa Uhifadhi Ngorongoro washikiliwa kutokana na kifo cha fundi gereji Ngorongoro
Maafisa hao wamefika msibani kwa lengo la kutoa pole kwa familia pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa mazishi ya kijana huyo, yanayotarajiwa kufanyika leo Agosti 14, majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mrombo.
Baba mzazi wa Sefu amezungumza kwa uchungu kuhusu namna alivyopokea taarifa za kifo cha mwanawe, akisema taarifa hizo zimemuumiza sana. Ameitaka Serikali kuhakikisha haki inatendeka na wote waliohusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Source: Royalonline tv