JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha Usalama Barabarani wametaja barabara zitakazotumika katika tamasha la Landrover litakaloanza kuanzia Oktoba 12, 2024 Mkoani Arusha huku likisema limejipanga vyema kuhakikisha linafanyika kwa amani na utulivu.
Akitaja njia hizo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema washiriki wa tamasha hilo watajipanga barabarani maeneo ya King’ori wilayani Arumeru alfajiri ambapo kuanzia muda wa saa moja asubuhi msafara wa magati hayo utaondoka kuelekea katika viwanja vya Magereza Kisongo.
SSP Zauda ameendelea kufafanua kuwa mara baada ya kuondoka King’ori utaenda hadi katika mataa ya Philips na ukifika hapo utaelekea mzunguko ‘roundabout’ ya Impala hadi mzunguko wa Saa maarufu ‘clocktower’.
Mkuu huyo wa usalama barabarani amesema baada ya kufika mzunguko wa mnara wa saa, msafara utapita barabara ya Sokoine -metropol na kupinda kulia katika barabara ya Swahili hadi Mzunguko ‘roundabout’ ya Mnara wa Mwenge na kuelekea hadi kwenye mataa ya kuongoza magari ya Stendi kuu.
Msafara huo utaelekea Mianzini kupitia Roundabout ya Florida, na utakapofika Katika mataa ya Mianzini utaenda hadi Ngaramtoni katika Makutano ya barabara ya Afrika Mashariki ‘Bypass’ na kupinda kushoto kuelekea Roundabout ya Kisongo na hatimae kufika katika viwanja vya magereza
Aidha SSP Zauda ametoa wito kwa wananchi hususani watakaotumia barabara za katikati ya mji kutumia niia mbadala huku akiwahakikishia kuwa Askari watakuepo barabara kuwaelekeza barabara za kupita kuepusha foleni ambazo zitajitokeza.