Polisi: Bado tunasubiri Polepole aripoti Ofisi ya DCI; taarifa za kutekwa kwake tumeanza kufanyia kazi

Polisi: Bado tunasubiri Polepole aripoti Ofisi ya DCI; taarifa za kutekwa kwake tumeanza kufanyia kazi

Wote police wanaliwa viboga na wenyewe.....Tutawaashibu kweli kweli...
 
Hiyo maana yake ni kusema hawapo nae bila kusema hawajamchukua wao.

Ndo hapa sasa mimi huwa nagombana na wa Tz wenye tabia za kinafki na uoga kama nyumbu, mtu akijitoa kwaajili yao huwa wanajaza comments na likes kuonyesha wapo nae ila mtu huyo akitendewa unyama wa Tz huwa hawako tayari kutoa hata tone moja la jasho kwaajili ya huyo mtu achilia mbali damu hata tone la jasho hawatatoa kwaajili ya huyo mtu.

Mimi nitaendelea kugombana na keyboard warriors wote popote pale nitakapokutana nao humu jf maana ni wanafiki na ni nyumbu hawana wanachoweza kufanya kwaajili ya anaewatetea.

Hata Lissu kaachwa mahabusu miezi 6, Mbowe, Soka, Mdude pia wameachwa na hawa wanafiki wa mitandaoni.
Hoja yako ina uzito lakini inahitaji muktadha mpana zaidi.

Ni kweli tunahitaji watu jasiri wanaosimama kwa ajili ya haki, lakini pia hatuwezi kupuuza mazingira ya hofu na ukatili yaliyotengenezwa na mfumo.

Unaposema keyboard warriors ni wanafiki au nyumbu, ni kama unafumbia macho ukweli kwamba wengi wao ni raia wa kawaida wasio na ulinzi wala nguvu ya kukabiliana na watu kama Mafwele ambaye hata viongozi wa juu yake wanadaiwa kumuogopa.

Ujasiri wa mtu haumaanishi kutokuwa na hofu, hasa mbele ya silaha na mfumo usiojali usalama wa raia.

Hatuwezi kumtaka mama wa familia, kijana wa mtaani au mfanyakazi wa kawaida ajitose mbele ya watekaji wenye silaha bila ulinzi wowote. Hilo siyo uoga, bali ni uhalisia wa mazingira ya hatari.

Lakini nakubaliana na wewe kwenye kipengele cha raia kushindwa kuchukua hatua pale wanaposhuhudia utekaji hadharani.

Hapo ndipo tunapopaswa kujiuliza: je, tumefika mahali ambapo hofu imezidi utu? Kama jamii, tunahitaji kuamka lakini si kwa lawama bali kwa kujenga uelewa, mshikamano na mifumo salama ya kupinga uonevu.

Kwa sasa, keyboard warriors ni sehemu ya sauti ya upinzani. Wanaweza wasiwe na uwezo wa kuzuia utekaji, lakini wana uwezo wa kueneza taarifa, kuhamasisha mjadala na kushinikiza mabadiliko. Tusiwadharau, bali tuwatie moyo wa kuendelea kupaza sauti kwa sababu hata tone la sauti linaweza kuwa mwanzo wa mawimbi ya mabadiliko.
 
Hisia zinaniambia ya kuwa, POLEPOLE ATAKUWA MTU WA MWISHO KUTEKWA KABLA TAIFA HALIJAKOMBOLEWA!

Polisi wanakana kumshikilia ili WAMPOTEZE KIMYA KIMYA, Jambo ambalo halitakuwa jepesi kama wanavyojidanganya!
Kuna wachache sana watakuelewa lakini kiintelijensia mission iko 90% to completion na tunahitaji kuanza kusali sala za kumshukuru Mungu kwa kuruhusu Pole pole achukuliwe leo Ili Tanganyika ipone.

Sisi wakristo tunamshukuru Mungu pia kwa kumruhusu mwanae akamatwe na afe kwa ajiri ya ukombozi wetu.

Kwa waliowahi kusoma kitabu cha novel cha A Grain of Wheat pia watakuwa wanaelewa kwamba Ili mbegu iweze kuchipua na kuzaa matunda ni sharti ipitie hatua kadhaa muhimu. Mbegu moja inatuzalishia magunia ya mbegu
 
Hii nchi haijali uhai wa mtu kwaiyo ukiamua kujitoa muhanga fanya in full mode kama ndugu yetu yule alieshusha polisi 8 futi sita
 
Back
Top Bottom