Polisi: Binti aliyefanyiwa ukatili yupo salama salimini, puuzieni wanaosema amekufa

Source ni Millard Ayo japo sina uhakika sana mwenye uhakika atujuze
View attachment 3063647
Yaani Kesi ( Tuhuma ) iwahusishe Watu wa Sekta Muhimu halafu ambao wanatakiwa pia Kuichunguza wawe ni hao hao Watu Muhimu kisha Wahusika wapatikane kisha aitwe na atoe Ushahidi Kamili halafu Wahusika wakaozee Jela Maisha au Wanyongwe na Yeye abakie Uraiani? Ni lazima tu UMAFIA mkubwa wa Kuratibiwa vyema ufanyike / ufanywe ili Yeye Mmoja aondoke na USHAHIDI ufutike kwani mwenye Kuujua Ukweli ni Yeye mhusika na siyo Sisi WANAFIKI na wapiga Kelele humu Mitandaoni.

Imeisha hiyo......!!
 
Inawezekana lengo la uzushi ni kupata mwanya wa kuweka picha yake kama tunavyoiona sasa, serikali imchukulie hatua aliyeweka picha ya huyo binti kama muendelezo wa kumnyanyapaa.
 
Ila polisi wa Tz kila siku wanadhidi kujitia aibu na kuitia aibu serikali. Jana mkuu wa Wilaya katuma media anatafutwa bint akaja na kusema huyo binti hajulikani wala Temeke hawamjui watu wakaanzisha haya mambo sasa halafu wanakuja polisi na wanasema yupo hai, ok yupo yuko wapi? polisi kama wamejuwa yuko basi wanaye wao. Polisi fanyeni kazi kwa weledi sio kwa mihemuko ya social media, dunia imebadilika sana ndio maana mnatakiwa kuwa wepesi wa kutoa taarifa sahihi sio lazima maelezo ya ndani ya upelelezi lakini yako mambo ni lazima muwe wa kwanza kuyaweka hadharani.
 
Jamaa walikosea sana kutoa taarifa kua wanafuatilia hili suala from the firstplace, ilitakiwa waingia front kimya kimya kukamata hao jamaa.

Sasa kazi yao ishakua ngumu maana jamaa wanaishi mafichoni
 
Sasa mtu abakwe/Alawitiwe na aendelee kuonekana mtaani how comes? Wakija kupiga vingine 😄

Usikute binti wa watu kajificha hataki kuongea hata na wazazi wake kwa aibu.

Haya mambo omba uasikukute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…