Mjukuu wa kigogo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 445
- 1,094
Hili sasa ni janga kuu hapa Bunda. Unapoamka alfajiri unakutana na makundi ya watoto na vijana wamebeba shehena za vyuma kwenye mifuko na maboksi yao. Wanavitoa wapi? Mwisho wa safari zao huwa ni kwa wachuuzi wa vyuma ambao kwa bahati mbaya sana hawabagui vyuma aina ya vyuma chakavu wanavyotakiwa kuchukua. Wao ni chuma chochote kiletwacho kazi na dawa!
Matokeo yake ni nini? Sasa hivi kwenye Taasisi nyingi miundo mbinu ya mabomba na umeme imeharibiwa na kuibiwa. Kwenye familia nyingi pia uharibifu unafanyika! Matokeo yake serikali inaingia gharama kubwa sana kufidia miundombinu iliyoharibika lakini pia familia zinakuwa zinarudishwa nyuma kimaendeleo!
Uchunguzi wa kina ufanyike kwenye maghala ya hawa wanunuzi ili vyuma vilivyonunuliwa kinyume cha sheria vitolewe maelezo ya kina na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Katika kukomesha hili urahisi unaweza kupatikana kwanza kwa kumbana mnunuzi ndipo hatua za kuwabana wauzaji zifuatie.
Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli....