Polisi Dodoma yamshikilia Mlinzi wa Kanisa kwa tuhuma za mauaji ya msanii Man Dojo

Polisi Dodoma yamshikilia Mlinzi wa Kanisa kwa tuhuma za mauaji ya msanii Man Dojo

Ni mazingira yapi alikuwepo huyo Mandojo mpaka akaitiwa mwizi na kupigwa? Mbona hili watu wanalikwepa, inabidi tuambiwe ili wengine wajifunze kujiepusha kuhisiwa vibaya.

Unless tuambiwe huyo mlinzi ni kichaa kilimpanda kichwani, ila mwenye akili timamu kuna dalili mbaya aliziona na kuhisi isivyo. Kosa lilikuwa kumpiga ila angekakatwa yawezekana alikuwa na tresspass. Kanisa ni sehemu ya mtu yeyote kwenda, sasa iweje uwe uwanjani au kanisani uitiwe mwizi.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Raphael Ndamahnwa ambaye ni mlinzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu wote lililopo Nzuguni B kwa ajili ya mahoniano, kufuatia kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya Joseph Francis maarufu Mandojo kilochotokea Agosti 11, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Anania Amo amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumuhoji mlinzi huyo kuhusiana na tukio hilo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya chunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake.
View attachment 3068647
RIP Mandojo.

Unamuuaje mtu kwa kumdhani mwizi kanisani, sehemu ambayo hata mwizi wa kweli akiwa anakimbizwa na watu anaruhusiwa kukimbilia na kutetea asiuawe?
 
RIP Mandojo.

Unamuuaje mtu kwa kumdhani mwizi kanisani, sehemu ambayo hata mwizi wa kweli akiwa anakimbizwa na watu anaruhusiwa kukimbilia na kutetea asiuawe?
Hahaha 😂 kanisani ushawahi kulinda? Jichanganye uitiwe Mwizi alafu kimbilia kanisani ukutane na walinzi wa kanisa hawajalipwa tarehe ya 50 inaelekea tarehe ya 60 malipo yasiyokidhi mahitaji yao uone wanachokufanya km hawajakugeuka Pilau la Pasaka
 
Mtoto Wewe ambae umejoin Juzi JF Mimi ni Mkubwa wako maana nimekutangulia kukata utepe tena utulie sichelewagi kutembeza makonzi kwa madogo wasumbufu
Nimejoin juzi ila naijua mitaa ya jf usipime
 
Hahaha 😂 kanisani ushawahi kulinda? Jichanganye uitiwe Mwizi alafu kimbilia kanisani ukutane na walinzi wa kanisa hawajalipwa tarehe ya 50 inaelekea tarehe ya 60 malipo yasiyokidhi mahitaji yao uone wanachokufanya km hawajakugeuka Pilau la Pasaka
Mkuu,

Mimi nafanya hesabu za ku derive formulas za Pure, wewe unasumbuka na Basic Applied Math.

Hatuwezi kuelewana.
 
Nilisikia mara ya kwamba mara ya mwisho alikuwa anakunywa pombe sana, hivyo siku hio alimuaga wife wake anakwenda kutubu kanisani aachane na mambo ya pombe n.k...
Kumbe ndio wanaenda kumuua? Walinzi wa kanisa wakishalamba kitu cha Ukoo wa Yesu wanakua hatari sana kwa afya ya kelele za Mwizi
 
Kumbe ndio wanaenda kumuua? Walinzi wa kanisa wakishalamba kitu cha Ukoo wa Yesu wanakua hatari sana kwa afya ya kelele za Mwizi
Walinzi wengi hawana ethics za kazi zao... Huyo ni mandojo.. ina maana kuna wengi tu ambao sio maarufu walishapotezwa kwa kuitwa wezi na kuuawa pasipo hatia.
 
Penye ukakasi ni hao waumini waliomsaidia mlinzi kumpiga mwizi. Kanisani ni sehemu ya kwenda kutubu ambapo huwa tunasema "utusamehe makosa kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea".. sasa ndugu zetu wakatoliki huwa ni tofauti? Itakuwa ngumu kuzuia mashambulizi ya bibi FaizaFoxy
 
Uislam mwema sana.

Walivyokuwa wanauwana Rwanda na Burundi walikuwa wanakimbilia misikitini kujiokoa.
 
Uasi mwingi unaendelea hapa Tanzania kanisa lipo kimya ,inawezekana abduli amewapa njuruku wakae kimya
 
Penye ukakasi ni hao waumini waliomsaidia mlinzi kumpiga mwizi. Kanisani ni sehemu ya kwenda kutubu ambapo huwa tunasema "utusamehe makosa kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea".. sasa ndugu zetu wakatoliki huwa ni tofauti? Itakuwa ngumu kuzuia mashambulizi ya bibi FaizaFoxy
Mashambulizi ya ni tena kutokea kwangu?
 
Back
Top Bottom