Inaonekana poti kachanganya vipengele vya Sheria ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Usalama wa Taifa bila kutoa ufafanuzi wa kutosha. Kila sheria ina mazingira yake ya utumiaji.
Adhabu aliyoitaja ya faini ya shilingi milioni tano hadi ishirini au kifungo cha miaka mitano si sahihi. Adhabu ya kosa la kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ni faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu, au vyote kwa pamoja.
Mwamba ajitahidi asichanganye sheria