Polisi: Hakuna Mchimbaji aliyefariki kwenye Machimbo ya Msasa, Geita, baada ya maduara kuanguka

Polisi: Hakuna Mchimbaji aliyefariki kwenye Machimbo ya Msasa, Geita, baada ya maduara kuanguka

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Baada ya kusambaa kwa tetesi zinazodai zaidi ya watu 200 wamefariki kwenye machimbo ya Msasa Geita, jeshi la Polisi limekanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha.

Tetesi za tukio hili zipo hapa >>> Wachimbaji zaidi ya 200 wahofiwa kufariki huko Geita Machimbo ya Msasa baada ya madaura kuanguka

IMG_20260329_202948_468.jpg
 
Yaani alipomaliza tu kukagua na kuwasanua wenzake yakaporomoka yote manne? What a coincidence!


Breaking bad
 
Hao ni wa kuwapuuza tu, hakuna tangazo la police wa tanzania la kusoma mpaka mwisho
 
Watanzania tumeshazoea kuonewa.
Ni uonevu wa mchana kweupe na wala hakuna anayejali, sio muoneaji wala anayeonewa.

Yaani ndani ya Kijiji X, mwanakijij fulani katika harakati zake za kilimo ndani ya shamba lake mwenyewe, anakuja kugundua kwamba kwenye shamba lake muna dalili za uwepo wa dhahabu..........anajaribu kuchimba, mara kweli, anakutanayo....
Cha ajabu, atafukuzwa hapo shambani atake asitake.........ataambiwa tayari eneo lake lina mtu na alishalikatia leseni miaka 10 iliyopita.
Sasa Jiulize, aliwezaje kulikatia leseni eneo asilolimiliki?
Je aliwezaje kujua kama kuna dhahabu pale wakati hajawahi wala kukanyaga pale?
Hii ndio Tanzania......
Sasa haya ndio yanayoendelea sasa kule Coco beach
 
Zipo Taarifa kwamba Mgodi unaomilikiwa n.a. Mkuu wa Mkoa wa Geita umeporomoka na kuua zaidi ya wachimbaji 100.

Na kwamba Polisi wa FFU wamezingira uokoaji Ili kuficha idadi ya maiti zinazoopolewa

Mwenye Taarifa kamili atuwekee hapa.
 
Watanzania tumeshazoea kuonewa.
Ni uonevu wa mchana kweupe na wala hakuna anayejali, sio muoneaji wala anayeonewa.

Yaani ndani ya Kijiji X, mwanakijij fulani katika harakati zake za kilimo ndani ya shamba lake mwenyewe, anakuja kugundua kwamba kwenye shamba lake muna dalili za uwepo wa dhahabu..........anajaribu kuchimba, mara kweli, anakutanayo....
Cha ajabu, atafukuzwa hapo shambani atake asitake.........ataambiwa tayari eneo lake lina mtu na alishalikatia leseni miaka 10 iliyopita.
Sasa Jiulize, aliwezaje kulikatia leseni eneo asilolimiliki?
Je aliwezaje kujua kama kuna dhahabu pale wakati hajawahi wala kukanyaga pale?
Hii ndio Tanzania......
Sasa haya ndio yanayoendelea sasa kule Coco beach
Ulime shamba tu ukutane na dhahabu ebu kuwa serious....
 
Back
Top Bottom