GE2025 Polisi: Hatutasita kumchukulia hatua atakayeenda kinyume kwenye kampeni

GE2025 Polisi: Hatutasita kumchukulia hatua atakayeenda kinyume kwenye kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
“Kamwe asiwepo mmoja wetu akawa chanzo cha kukiuka sheria, kanuni na taratibu wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni ili kuepuka vurugu au uhalifu wa aina yeyote ile kutokea.”

Hiyo ni kauli ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyotolewa kupitia msemaji wake, David Misime leo Jumatano Agosti 27, 2028 ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kuanza kwa kampeni za wagombea wa urais, ubunge na udiwani kesho Agosti 28, 2025.

Soma pia: Mbona ni kama Rais Samia kaanza kampeni tayari?kwa nini hachukuliwi hatua na mamlaka?



Kauli hiyo inakuja huku joto la uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 likizidi kupanda ikiwemo kuanza kwa kampeni hizo, ambapo tayari vyama vinavyoshiriki uchaguzi vikitangaza kuanza mikutano ikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoanza kesho Kawe Dar es Salaam.

Kupitia taarifa hiyo Polisi imewajulisha wananchi na wadau wote kuwa, ipo tayari na imejiandaa vizuri ipasavyo kuhakikisha wanaendelea kuimarisha usalama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni.

“Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wagombea na wafuasi wao na wananchi wote kwa ujumla, kukumbuka jukumu la kudumisha amani, utulivu na usalama ni letu sote kama Watanzania.”

“Tunatoa wito kila mmoja azingatie ratiba na muda wa kampeni aliopangiwa ili kuepuka mivutano, migongano, migogoro au uhalifu kutokea kwani hatutasita kumchukulia hatua kama sheria za nchi zinavyoelekeza,” imeeleza taarifa ya jeshi hilo.
 
Back
Top Bottom