Polisi Ileje wakabidhiwa gari kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu

Polisi Ileje wakabidhiwa gari kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban amemkabidhi gari mpya aina ya Toyota Hilux Double Cabin Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ileje kwa ajili ya kuzuia uhalifu ambalo litatumiwa na Kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai Wilaya Ileje.

Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 06, 2025 katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, huku ACP Akama alitumia muda huo kumtaka dereva wa gari hilo kulitunza kwa uangalifu mkubwa ili liweze kutoa huduma kwa muda mrefu zaidi.

Aidha, ACP Akama ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kulijali Jeshi la Polisi na kutoa gari hilo.
snapins-ai_3737592158715968988.webp
snapins-ai_3737592158707579335.webp
 
Back
Top Bottom