Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Hii tabia ya watu kuweka taa kali za China kwenye magari imezidi mipaka sasa. Ni wakati muafaka Polisi waanze kukamata magari na bodaboda wanaofunga taa hizi.
Na hii ni tabia moja mbaya ya ubinafsi sana (selfish and self centred). Unaweka taa kali ili wewe ndio uone barabara vizuri - na hao wengine unaowa-blind je, umefikiria athari kwao ukiwasha taa zako?
Halafu kuna baadhi ya madereva wajinga sana hawatumii dim light wanapokuwa barabarani - kila wakati wako high beam (full lights)
Na kuna madereva washamba fulani wao wanatumia fog lights (zina unjano hivi) wakati hakuna mvua wala ukungu.
Na kuna mtindo wa kuweka hizi taa za kuwaka kimulimuli (throbbing lights). Wengi wanaweka kwenye breki na bajaji na bodaboda wanajiwekea tu. Zina athari mbaya kwa watu wenye kifafa - Polisi piga marufuku!
Haya yote mnayofanya ni makosa. Taa kubwa za mbele hairuhusiwi kuweka balbu za zaidi ya Watt 50. Huruhusiwi kutumia foglights wakati hakuna mvua wala ukungu. Manaumiza watu macho!
Ni hapa Tanzania tu Polisi wamekuwa busy na waandamanaji walizembea kufuatilia hili, lakini sasa wameanza kuamka. Afadhali.