Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi. Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.
Lazima maslahi ya wanawake kwenye majeshi hayo yafanane maana hapo unakutana na WP anakung’ang’ania ili uwe nae walau asogeze siku, utakuta mnabaki mnalaumu ooohhh askari ni majambazi kumbe ujambazi mmeuandaa wenyewe yeye yuko station labda benki analinda mabilioni anaona transaction za kibiashara kubwa kubwa then mwisho wa mwezi anapata laki nne au tano huyu mtu akipata upenyo akajua una pesa lazima akuue tu hana jinsi.
Uhamiaji hapo unaandaa ukaguzi wa mizigo ndio unazalisha na wadokozi iwe mipakani au airport. Atakagua aone kitu kizuri unadhani atakiacha kweli au atapewa rushwa watu wavuke kimagendo unadhani ataiacha hiyo rushwa?
Zimamoto huko ndio kuna balaa yaani mishahara mibovu haijawahi kutokea, hawaendi mafunzo maalumu kwa wakati, hawana drones za kuzima moto kwenye majengo marefu, yaani kila wilaya inatakiwa ipate gari la zimamoto lakini pia wawe na walau kisima kimoja kirefu cha maji yasihokauka ili ikitokea tukio wachukue maji hapo sio waanze kuzunguka bila plan, hawa watu hufanya kazi kwa stress sana.
Jeshini ndio yale yale ni vile hawasemi lakini wameandamwa na mikopo isiyo na idadi na wapiganaji wetu ukiongea nao pembeni wanalaumu sana juu ya maslahi yao.
Reforms kubwa za maslahi ya hawa watu zinatakiwa hapo tutawafanya wawe weledi, na Tamaa ya Rushwa itapungua japo kidogo.
Serikali wajalini hao watu ili wapunguze hata uonezi kwa raia wetu wa kawaida.