Polisi, Jeshi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto mishahara yao ni midogo, Serikali muwaongezee

Polisi, Jeshi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto mishahara yao ni midogo, Serikali muwaongezee

Dah kazi zote muhim na ningumu ila kwa JW dah hapana asee...

Ukienda mipakani ndo utajua hii nchi ina Jeshi na Matambo ya kutosha asee yasikie tuu kwenye Tv na sio karibu yako au usilengwe wewee

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Pesa yao Ni ndefu Sana ... ..ndio.maana wanakubali kadhia zote.

Na ndio maana wanaongoza kwa Yale Mambo flani!
 
Utumishi wa sasa ni kama tunavolunteer . Masaa nane ya kazi unachoingiza hakiwezi somesha watoto, kujenga, etc japo wasio na ajira wanàtamani kazi bora ujiajili hakuna anaekucontrol

Ndio maana tunawapigania ili muongezewe mshahara na marupurupu mengine
 
Mpaka gani, Namanga, Tunduma, Rusumo, Kabanga, Mutukula, Munanila, Tangazo, Mtambaswala, indian ocean shore au upi hasa ndio maana tunasema kwa kazi za wapiganaji wetu lazima waongezewe maslahi
Kabisa mi hili hata sipingi kabisa anii.

Kule mpaka akili zao kama Fyatu tuu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Tumeanza na hao kuchokoza maada huko kuna madaktari MD analamba kama 800k hivi, manesi, walimu huko wanacheza na 400k hadi 600k hao nao wakuonewa huruma kuna watumishi wa umma hata afanye scrub vipi bado ngozi inakua imekakamaa sababu ya stress na mawazo hasa kwa hizo salary mfano maisha ya Dar anayamudu vipi ndio huchelewi kukuta watumishi wa umma nao wanajiuza kama kawaida tu
Wa kuonewa huruma nj wale ambao hawana anira,wanatamani hata nusu ya hiyo laki 8
 
halafu Jeshi wala hawana mishahara midogo! Mungu anawaona! kujipendekza kwa Rais wamejazwaa tena kwenye kazi za uraiani! uroho mbaya sana! kuna mmoja alitimuliwa STAMICO hapa! kwa kuwa na low IQ, kuona wafanyakazi kama watu wa chin tu! akakata stahiki zao wakati yeye anasafiri hadi nje ya nchi! Akatimuliwa kurudishwa jeshini huko! dhambi zinawatafuna wengi wanaishia maisha ya shida tu ingawa wana kiinua mgongo kikubwa
Bro wanajeshi kupewa kazi uraiani sio dhmbi,sababu wana elimu za kiraia pia.

Pia ndio majukumu ya wanajeshi hayo wakati wa Amani
 
Ndio maana tunawapigania ili muongezewe mshahara na marupurupu mengine
Mnaandaa taifa mfu.

Nusu ya makusanyo kwa mwezi yanatumika kulipa mishahara, robo kulipa madeni, robo Maendeleo.

Sasa mnataka kuikomba na hiyo robo ya maendeleo
 
Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi.
Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.
Lazima maslahi ya wanawake kwenye majeshi hayo yafanane maana hapo unakutana na WP anakung’ang’ania ili uwe nae walau asogeze siku utakuta mnabaki mnalaumu ooohhh askari ni majambazi kumbe ujambazi mmeuandaa wenyewe yeye yuko station labda benki analinda mabilioni anaona transaction za kibiashara kubwa kubwa then mwisho wa mwezi anapata laki nne au tano huyu mtu akipata upenyo akajua unapesa lazima akuue tu hana jinsi.
Uhamiaji hapo unaandaa ukaguzi wa mizigo ndio unazalisha na wadokozi iwe mipakani au airport Atakagua aone kitu kizuri unadhani atakiacha kweli au atapewa rushwa watu wavuke kimagendo unadhani ataiacha hiyo rushwa?
Zimamoto huko ndio kuna balaa yaani mishahara mibovu haijawahi kutokea, hawaendi mafunzo maalumu kwa wakati, hawana drones za kuzima moto kwenye majengo marefu, yaani kila wilaya inatakiwa ipate gari la zimamoto lakini pia wawe na walau kisima kimoja kirefu cha maji yasihokauka ili ikitokea tukio wachukue maji hapo sio waanze kuzunguka bila plan, hawa watu hufanya kazi kwa stress sana.
Jeshini ndio yale yale ni vile hawasemi lakini wameandamwa na mikopo isiyo na idadi na wapiganaji wetu ukiongea nao pembeni wanalaumu sana juu ya maslahi yao.
Reforms kubwa za maslahi ya hawa watu zinatakiwa hapo tutawafanya wawe weledi, na Tamaa ya Rushwa itapungua japo kidogo.
Serikali wajalini hao watu ili wapunguze hata uonezi kwa raia wetu wa kawaida.
Unapendekeza waongozewe bei gani?

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu polisi nadhani trafiki wapunguziwe mshahara maana jamaa hawakosi 50 minimum kwa siku.
Na trafiki wa Kasulu, Misenyi , Tabora au Kilombelo nao hukusanya 50 kwa siku?
 
Na trafiki wa Kasulu, Misenyi , Tabora au Kilombelo nao hukusanya 50 kwa siku?

Trafik wa Kasulu hadi nguo zao ni nyekundu kama vumbi lao, maisha ya trafik yapo Mbeya, Igunga, manyoni, nzega, njombe, kibaha hadi mlandizi, Arusha to moshi, moro to Dodoma, mbeya to kyela, mbeya to Iringa
 
Kwa JWTZ hapo uongo. JWTZ wana mishahara mikubwa, sema tatizo wanaishi kwa mashindano.

Baadhi hawana stadi za maisha nje ya kuzifahamu silaha, na ndio hawa wanaosumbua watu mtaani kwa maisha magumu.

Mwanajeshi akiona mwenzake amenunua sijui Alteza, na yeye anaenda kukopa ananunua. Mwanajeshi akiona mwenzake kajenga lijumba likubwa, na yeye anenda kukopa anajenga.

Ila ukikuta mwanajeshi anaishi maisha yake halisi, hawezi kufulia na tena atakuwa ana maendeleo makubwa kwa sababu wanapata mishahara mikubwa sana.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Msiwasahau na watumishi wa TRA nao waongezewe mshahara..wanaishi maisha magumu sana 😰😰
 
Utumishi wa sasa ni kama tunavolunteer . Masaa nane ya kazi unachoingiza hakiwezi somesha watoto, kujenga, etc japo wasio na ajira wanàtamani kazi bora ujiajili hakuna anaekucontrol
Acha kazi mkuu...wapo wanaokitamani hata hicho kidogo unachokipata wewe
 
Back
Top Bottom