Polisi, Jeshi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto mishahara yao ni midogo, Serikali muwaongezee

Inatosha sana wanalipwa mishahara na posho Kila katikati ya mwezi
 
Hao watch dog Takukuru na Tiss wasipolipwa vizuri tegemea Mambo kuwa mabaya zaidi coz njaa itawafanya kushindwa kuziba mianya ya upigaji
 
Hahaha wanapenda alteza kinomaa
 
Jw wana mishahara mikubwa sana kama hufahamu.Wenye njaa hapo:ni polisi,magereza,uhamiaji na Zimamoto.

Ila mimi ningekuwa Rais ningewaongezea mishahara polisi maana kazi yao ni kubwa kuliko hao wengine,polisi kazi yake inaendana na ile ya Jwtz kule mtwara ndio nilithibitisha kwamba polisi nao wana mziki mzito.

Askari wa kuzima moto, magereza na uhamiaji kupata mshahara sawa na polisi ambaye yupo kwenye higher risk ni dharau kubwa kwa polisi wetu.
 
Siku nyingine kabla ya kuandika kitu fanya utafiti kwanza.

Polisi wote Tanzania kila mwezi wanalipwa posho ya shilling laki tatu bila kujali cheo hii ni nje ya mshahara.

Hiyo posho tu ya Polisi ndio mshahara wa watu wengi kwenye sekta binafsi na wengine ni chini ya kiwango hiko.

Punguza kula makande ili usiwe unaleta mashuzi jukwaani.
 
Nakazia mkuu..wanavunjiana Bei kwa mwanamke... Yuko radhi ampe mshahara wote wa mwezi mradi tu amchukue...halafu akajisifu kambini kwamba tayari Fulani Nisha chapa.. .. na pombe.. ..wengi wao Wana ulimbukeni flani..
 

Wewe umekula njugu mawe
 
Mshahara na posho ya askari asiye na cheo katika majeshi yote nchini ni zaidi ya mshahara wa Mhasibu mwenye Shahada ya kwanza anayelipwa kwa scale pendwa ya TGS D.

KWA UFUPI MISHAHARA MIZURI iko kwenye mashirika ya umma. Kuna mashirika mtu mwenye diploma tu tena anayeanza kazi anamzidi mshahara Mhandisi wa muda mwingi yaani senior Engineer wa TBA, TEMESA, SIDO n.k
Hii nchi imenajisiwa na viongozi haramu wasio na utu.

Mimi binafsi nitaendelea kujiongeza niwapo kazini liwalo na liwe, kufa maskini huku majirani wakijua kuwa ni mtumishi wa umma never
 
Kila mtumishi ni muhimu katika nafasi yake haijalishi anafanya kazi gani na wapi, wanatakiwa wapewe mishahara kulingana na hali ya maisha ilivyo kwa sasa maana masoko wanayokwenda ni hayo hayo, shule wanazosomesha watoto ni hizo hizo , na hata hewa wanayovuta ni hiyo hiyo hakuna sababu ya kuweka matabaka.
 
Ukilinganisha na mishahara wanayojilipa Wabunge na viongozi wengine,Naunga mkono hoja.
 
chotera watumishi wote wapewe stahiki sawa mbona unakuwa na ubinafsi
Kazi ya Utumishi wa Umma ni kazi ya kujitolea, na si kazi ya kwenda kujitajirisha, yoyote anaetaka utajiri Ruhksa kwenda kufanya Biashara zake kwa uhuru,na atuachie Utumishi wetu, Wazalendo wa kufanya kazi wapo wengi tu mtaani!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Uhalifu ni tabia binafsi hauna uhusiano na kipato
 
 

Mishahara mikubwa sana kwako ni kiasi gani?
 
Na wao waongeze weledi was kazi kwanza
 
Unaweza kuwa upo sawa! Lakin kwa upande mwingine nauona mtazamo wako sio sahihi, Ukisema tumuongezee askari mshahara kwasababu tu analinda fedha za benk , Vipi Watendaji wa afya wanaokoa maisha na uhai wa wananchi wetu? Vipi Waalimu wanaoelimisha na kuwezesha watoto wasiojua chochote lakini wanafika mahala wanafahamu kusoma na kuandika?

Nafkiri kampeni inatakiwa kupigwa kwa watumishi wote ili kila mmoja awe na nafuu ya maisha! Bora hata ungelea sekta nyingine lakin kama ni askari tayari wanalipwa posho za lindo nje ya mshahara na wanajua kweli kuzisaka kutoka kwa raia, kama hulijuwi hilo uliza wafanya biashara hasa wanaosafirisha mizigo masafa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…