Polisi, Jeshi na usalama tendeni haki kwa manufaa ya taifa!

Polisi, Jeshi na usalama tendeni haki kwa manufaa ya taifa!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Polisi, Jeshi na usalama tendeni haki kwa manufaa ya taifa. Kama kweli mnapenda taifa hili simamieni haki na demokrasia. Waachieni Watanzania wachague watu wao kwa matakwa yao. Msiwaibie kura mafisadi.

Jeshi jiulizeni vizuri wenzenu wamekufa huko Congo Je ni lini hao wanasiasa wamewaongelea? Hao IGP wastaafu walio ongoza utekeji wizi wa kura na hata mauaji leo wako wapi inaelekea wanajuta huko waliko. Mnatakiwa kujiuliza mnafanya mambo kwa faida ya nani hasa. Wenzenu Zambia walikuwa wanatumia kuiba uchaguzi kuanzia waache na kuwa watu wa haki jamii yao inawaheshimu na nchi yao sasa ni ya kidemokrasia. Kwasasa nyie kwa jamii unaonekana kama wakandamizaji. wale ambao wamechaguliwa kwa wizi wenu wana dharau viongozi wenu hata ubunge wakienda kuomba walewale waliokuwa wanawatumia hawana imani na nyie. Aglaieni wakina Tibaigana, Kova na Mahita walishidwa kuingia kwenye siasa pamoja na waliofanya sasa wako wapi??. Lakini mki nyanyasa hata Mungu hawezi kuwabariki nyie binafsi huwezi kuibia watu kura na kusingizia viongozi. Au huwezi kuwauwa vijana halafu ukasingizia kutumwa!

1. Msiteke watu kwa kuagizwa
2. Msiwaibiwe chama chochote kura
3. Simamieni haki bila kujali vyama
 
Back
Top Bottom