Polisi jijini Dar wamjeruhi mtuhumiwa, yupo mahututi ICU

Huyo jamaa kanikwaza hata mimi! kama anahitaji kusaidia angemfuata hata inbox, sio kuuliza maswali ya kejeli, wakati mtu anatafuta haki na msaada wa kisheria
Pengine ndio kitengo cheke, na halafu yeye si mtu wa kukubali kukosolewa kwa makosa aliyofanya.

Aibu sana waafrika.
 
Jeshi letu la Polisi kuondokana na huu uonevu wanapaswa kuwa jeshi la kisasa, na siku zote jeshi la kisasa huwa linaendeshwa kisomi na wasomi. Afande SIRRO na kikundi chake wote ni wahuni hawana shule yoyote kulifanya jeshi la polisi kuwa la kisasa.
 
Raia wakati mwingine tunafeli hapo kwenye kuchukua hatua mapema, tunajisemea kuwa ''kesi ya nyani umpelekee ngedere!"
Kumbe wengine wala siyo ngedere bali nguchiro tu,, tunabaki kuwaogopea kwa mbali.
Bora mtu uingie kazini na kufeli kuliko kuogopea mbali.
 
Kuna mambo ya ajabu sana na mojawapo ni hili.Huyu mama awafungulie kesi mapema iwezekanavyo.Hawa viongozi wa polisi (IGPs)ni muda sasa wa kuangalia mienendo ya vijana wao.Haya ndio maadili waliyofundishwa polisi?Shame on them!
 
Sijui uhalisia wa story hii ila polis wa Tz ji changamoto kubwa sana katika jamii
 
Pole sana
Umenikumbusha story ya yule dada aliye kamatiwa Goba akapelekwa Kituo cha polisi Mburahati kisha akakutwa kafa akiwa lock up, kisha wakkasema kajinyonga alafu MNH wakasema amepata majerah kichwan

Tunaelekea wapi
 
Wanakuwa na waya wao wa nguzo za umeme.
Zile za aluminum.
Kuna kibaka mmoja alipigwa sarara moja la mgongo.
Aliita "mamaaaàaaaa"
 
Ii

Hii stori imepambwa sana. Huyo mtu mahututi 1% kupona aongee yote hayo!
Hali ya mgonjwa ubadilika Muda baada ya Muda.
uenda Sasa hivi yupo kwenye COMA.
alafu maandishi sio sawaa na kuongea uenda alikuwa anaongea kwa taabu. Lakini hapa kwenye maandishi unaona maneno yamenyooka
 
Wewe ni mgeni wa hili jukwaa? taarifa zote zinazokuja humu watu huwa wanajitetea walivyo zipata?

Mtu anafikisha ujumbe kwa uchungu na kutafuta haki, unaleta ujuaji!? hiyo story kwa kuisoma inaonekana sio ya kutengeneza, bado unaleta ujuaji!
Comment yake inasikitisha sana nimeisoma mara mbilimbili.Ni vyema kujifunza kujiweka kwenye position ya mtu mwingine unafikiri ingekuwa ndugu yake angesema hivyo?
 
Eeeh mwenyezi Mungu mpe nafuu mja wako,
Kufanya kazi kwa mazoea kuna athiri pakubwa sana sekta nyingi hapa nchin haswa ya ulinzi
 
Duh
 
Halafu baadae wanaenda kutoa ushahidi wa uongo mahakamani kwamba mtuhumiwa ni gaidi
 
Inawezekana kuna ukweli ila kwa namna story ilivyo inatia mashaka
 
kuweni makini katika kuwasilisha malalamiko yenu mnapohitaji msaada,ili isije onekana ni majungu.

wewe unasimulia kana kwamba ni shahidi namba moja wa tukio,kumbe umesimuliwa.

jf imejaa watu wa kila aina,wanawezasoma wakaiahia njiani wasione ukweli wa jambo husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…