Polisi jijini Dar wamjeruhi mtuhumiwa, yupo mahututi ICU

Polisi jijini Dar wamjeruhi mtuhumiwa, yupo mahututi ICU

ww hujitambui ,na akilini naona umejaa kinyesi

tumia akili sio matako kufikiri,ukitanguliza mihemko namna hii unapoteza haki ya msingi.

ndio nyinyi mnakuta askari anakamata mtu unazuia,wanakugonga unapewa na kesi ya kuzuia ukamataji.tuliza akili uache ashki.
 
Mtaji wa Polisi TZ, ni uzwazwa, upopoma,ujingaaa wa RAIA.

ujanja wa raia sio kubishana na polisi.

na kutafuta haki yako kwa utulivu,raia una mamlaka hata ya kuwasiliana na IGP ukamweleza kila kitu,sijui harakati kunuka huwa zinatokea wapi!!!
 
Wewe ni mgeni wa hili jukwaa? taarifa zote zinazokuja humu watu huwa wanajitetea walivyo zipata?

Mtu anafikisha ujumbe kwa uchungu na kutafuta haki, unaleta ujuaji!? hiyo story kwa kuisoma inaonekana sio ya kutengeneza, bado unaleta ujuaji!

kwamba kwa kuisoma tu tayari umeshajua sio ya kuitengeneza!!
kuulizwa source inategemea taarifa umeiletaje.

wenzako wanakwenda mbali zaidi,huyu simu moja tu akianza kuulizwa maswali uchungu wote unamwisha.

haya mjibie,yeye kasimuliwa na nduguye aliye ICU au ndio mhusika mwenyewe aliyepo ICU??au ndiye mama wa mhanga wa ICU?!
 
Yote haya kisa kutoongeza mishahara ya watumishi wa umma. Njaa imekuwa kali.
 
Polisi Goba, Dar, wajeruhi kwa kipigo, majeruhi yuko ICU, anapumlia mashine, madaktari wasema, kupona kwake utakuwa muujiza wa Mungu....

Jumatano, November 10, 2021, Polisi Goba walimkamata Issa Kassim (20), nyumbani kwao huko Goba kwa madai kwamba ameuziwa TV ya wizi, tukio ambalo mtuhumiwa alikana kulitenda.

Baada ya kumkamata waliondoka naye wakidai wanampeleka kituo cha polisi Goba, lakini kabla ya kufika huko kituoni walimuomba awapigie simu ndugu zake waweze kumuokoa.

Mtuhumiwa alipiga simu kwa mama yake akazungumza na mmoja wa polisi hao aliyefahamika kwa jina moja la Majuto.

Askari huyo wa jeshi la polisi kituo cha Goba, katika mazungumzo na mama wa mtuhumiwa huyo alimuomba atume Sh 800,000 ili kijana wake waliyemshikiria kwa tuhuma ya kununua TV ya wizi waweze kumuachia.

Mama wa mtuhumiwa aliomba apunguziwe dau hilo, badala ya sh 800, 000 atume 500, 000 , ombi lake lilikubaliwa akatakiwa atume hiyo laki tano.

Wakati biashara hiyo ikiwa kwenye mazungumzo, mtuhumiwa alikuwa akisikia, alimzuia mama yake kuwatumia polisi hao fedha yoyote kwani hajatenda kosa lolote, anasingiziwa tu.

Baada ya mtuhumiwa huyo kuzuia fedha kutumwa kwa polisi hao, polisi hao wakiongozwa na Majuto, na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Paul walimpiga sana, hasa maeneo ya kichwa kwa kutumia nyaya ngumu wakidai ni jeuri anazuia wao wasitumiwe fedha ili aachiwe.

Baadaye tena, akiwa tayari amepokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa polisi hao, alitakiwa kumpigia simu ndugu yake mwingine mwenye uwezo kifedha ili atume fedha hiyo aweze kuachiwa.

Alipigiwa simu binamu wa mtuhumiwa huyo aitwaye Tusekile Shadrack, ambaye alielezwa tukio hilo, na kutakiwa na afande Majuto, wa jeshi la polisi Goba atume fedha sh 800, 000 ili ndugu yake aweze kuachiwa na kufutiwa kesi inayo mkabili.

Ndugu huyo wa mtuhumiwa alimuomba polisi Majuto ampe namba yake ya simu amtumie fedha hiyo, aligoma kutoa namba yake, akamtaka atume kwenye simu ya mtuhumiwa au apewe namba ya wakala atoe kupitia huko, ilishindikana, fedha haikutumwa, mtuhumiwa alimzuia asitume chochote maana anasingiziwa tu, hajatenda kosa hilo.

Kipigo kwa mtuhumiwa kiliendelea, akiambiwa atakufa kwa sababu ya jeuri yake.

Alhamisi, November 11, 2021, asubuhi, Afande Majuto alimpigia simu Mama wa mtuhumiwa akimtaka afike Hospitali ya Mwananyamala haraka, hali ya mwanaye ni mbaya.

Mama huyo wa mtuhumiwa aliongozana na Tusekile kwenda Mwananyamala Hospitali, walipofika kweli walimkuta mtoto wao taabani, aliweza kuongea kwa shida sana!

"Nimepigwa sana, sidhani kama nitapona, niombeeni sana kwa Mungu, nimeumizwa, nakufa bila hatia yoyote, polisi wakiongozwa na Majuto, walinzi hawa wa raia na mali zao, wamenitesa vikali, wamenipiga kipigo kikali zaidi ya kile cha mbwa koko, wananiua eti kwa sababu nimewakosesha fedha za dhuruma walizotaka kuzipokea kutoka kwenu ndugu zangu, niombeeni, nami naomba, Mungu atanilipia" alisema Issa.

"Cha ajabu, yule mwizi waliyedai ameniuzia TV ya wizi aliachiwa, hakufika hata kituo cha polisi, aliambiwa tukiwa njiani tuna karibia kituo cha Goba atambaye, nakufa, nifikishieni salaam zangu kwa IGP Sirro, askari wake wanawatesa raia, wanawaua kwa kuwapiga wakitaka walipwe pesa kwa makosa ya kutengenezewa ili wapate fedha ya dhuruma, nakuacha mama, niombee kwa Mungu" aliongea Issa kwa majonzi makubwa.

Mwananyamala alifanyiwa kipimo cha cit-scan na MRI kichwani, wakadai mishipa ya mfumo wa fahamu kichwani imeathiriwa pakubwa, damu nyingi imevia, imeganda na kuikandamiza mishipa hiyo kwenye Ubongo.

Ilibidi haraka sana ahamishiwe Muhimbili, ambapo alipokelewa na yuko ICU, kwa mujibu wa maelezo ya madaktari bingwa wa Muhimbili wa mifumo ya fahamu ya kichwa(Neurosurgery) wanaomhudumia, wamesema kupona kwake ni asilimia moja, muujiza tu wa Mungu.!

Ndugu tumekata tamaa, hivyo tunaomba msaada wa kisheria na ushauri.
Maisha yao hayana tofauti na shetani wanalala rum moja na watoto kwenye nyumba za bati
 
Sasa mkuu c ungeandika Afande Majuto na Afande Paul wa kituo cha Polisi Goba kuliko kujumuisha Mapoti wote wa Dar!!,
 
Huyo jamaa kanikwaza hata mimi! kama anahitaji kusaidia angemfuata hata inbox, sio kuuliza maswali ya kejeli, wakati mtu anatafuta haki na msaada wa kisheria
Labda yeye ndiyo afande Majuto, maana siyo kwa maswLi ya PGO
 
Kwa uzoefu wa polisi wetu ninaoujua, hili Tukio litakuwa LA kweli tupu!! Tumuone afande Sirro atakavyookoa roho ya huyu Malaika inavyopotea
 
kwamba kwa kuisoma tu tayari umeshajua sio ya kuitengeneza!!
kuulizwa source inategemea taarifa umeiletaje.

wenzako wanakwenda mbali zaidi,huyu simu moja tu akianza kuulizwa maswali uchungu wote unamwisha.

haya mjibie,yeye kasimuliwa na nduguye aliye ICU au ndio mhusika mwenyewe aliyepo ICU??au ndiye mama wa mhanga wa ICU?!
Na hao ndugu waliopigiwa simu watoe pesa wapo ICU? Hacha mihemko
 
Street is saying that, out of all the high-powered, criminal street gangs, the largest and most dangerous of them all is the Police Department itself! This is due to police brutality and corruption in the force, and street says that this makes the police more criminal than the gangs themselves
 
Hapo hakuna mjadala. Jeshi la polisi watoe pesa ya kufidia hayo matibabu huyo mama asitoe hata senti tano yake....
 
Ukihoji hivi anaweza dhani upo kubishana nae.
Ameomba msaada wa kisheria na pengine hayuko sawa pyschologically.
Weka mood nzuri ya maswali ili kama una msaada umsaidie.
Kwani huyu ni nani tunayezungumza nae mpaka awe hayuko sawa kisaikolojia ninapomuliza maswali haya?
 
wabongo banah kwani mwenye asilimia moja ya kupona anatakiwa aongee maneno mangapi bosi kwa utaalamu wako?
Logically mtu ambaye ana 1% ya kupona hawezi kuongea lolote na pengine yupo kwenye coma yaani 99% amekufa. Kwahiyo huyu jamaa anaongea uongo.
 
Back
Top Bottom