Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Tumeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii ikitolewa taarifa ya kutaka kuupotosha umma kuhusiana na kifo cha Joseph Remigius, Miaka 52 mkazi wa Kijiji cha Karagara, Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa ametia nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa sahihi ni kwamba Oktoba 31, 2024 Joseph Remigius majira ya saa tatu usiku akiwa anatoka kwenye Bar waliyokuwa wanakunywa pombe akiwa amebebwa na bodaboda walipata ajali na baada ya ajali hiyo walipata msaada na kufikishwa katika Kituo cha Afya Minziro na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa.
Novemba 1,2024 majira ya saa kumi na dakika ishirini alfajiri ndipo zikapokelewa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Minziro kuwa Joseph Remigius amefariki dunia akiwa nyumbani kwake.
Hivyo hadi sasa kulingana na ushahidi wa mashuhuda wa ajali na waliompatia msaada na kumfikisha katika Kituo cha Afya Minziro, ajali ndiyo chanzo cha kifo chake. Endapo kuna mwenye ushahidi tofauti na huo wa mashuhuda wa ajali basi aufikishe Polisi ili ufanyiwe kazi.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Dodoma, Tanzania.
Pia soma ~ Missenyi, Kagera: Kada CHADEMA, Joseph Elemedius auawa akingojea Uteuzi kugombea Serikali za Mitaa