Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam: Binti anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai, hajafa kama ambayo imeripotiwa katika baadhi ya mitandao

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema Binti anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai, hajafa kama ambayo imeripotiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema tayari Jeshi hilo linamshikilia Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta wilaya ya Kinondoni anayedaiwa kusambaza taarifa hiyo mitandaoni.

Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema wanaendelea na uchunguzi kwa waliohusika na tukio hilo la ubakaji na ulawiti.

Soma Pia:
Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu'

TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam


Your browser is not able to display this video.
 
Mmmhh!
What is the hell about these people????

Yaani badala ya kuanza kuwakamata watuhumiwa waliofanya Uovu huo mbaya sana wameamua kuanza kumkamata Whistle blower aliyefichua taarifa hiyo ya Uhalifu??
Je, Jeshi la Polisi Lina maslahi yoyote yale dhidi ya hao Watuhumiwa??

Wananchi wanataka kupata taarifa juu ya hatua ambazo tayari Jeshi la Polisi limezichukua dhidi ya Watuhumiwa waliohusika na Ushetani huo.
Huu ukimya na kigugumizi walichonacho Jeshi la Polisi linaleta mashaka.

Whistle blower badala ya kulindwa anaadhibiwa??????!!?
 
Hahahaha nchi inaviongozi wapumbavu mno...hao vijana waliobaka ni wanajeshi na amini nawaambia hawatafanywa kitu chechote kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…